• HABARI MPYA

  Monday, February 06, 2017

  BASSOGOG MCHEZAJI BORA AFCON 2017

  MSHAMBULIAJI wa Cameroon, Christian Bassogog amekuwa Mwanasoka Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon mwaka 2017.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameisaidia sana Cameroon kutwaa Kombe la AFCON, baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri kwenye fainali jana Uwanja wa l’Amitie mjini Libreville na akatajwa Mchezaji Bora wa Mashindano na Kamati ya Ufundi ya CAF na kikundi cha Watathmini.
  ORODHA KAMILI YA WASHINDI AFCON 2-17
  Mchezaji Bora wa Mashindano: Christian BASSOGOG (Cameroon)
  Mchezaji Bora wa fainali: Benjamin MOUKANDJO (Cameroon)
  Tuzo ya Fair Play: Misri
  Mfungaji Bora: Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3
  Kikosi cha Mashindano cha CAF 
  Kipa: Fabrice ONDOA (Cameroon)
  Mabeki: Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)
  Viungo: Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri)
  Washambuliaji: Christian BASSOGOG (Cameroon), Junior KABANANGA (DRC)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BASSOGOG MCHEZAJI BORA AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top