• HABARI MPYA

    Friday, August 19, 2016

    HII NDIYO TAARIFA RASMI YA TFF KUHUSU HASSAN KESSY NA MKATABA WA SIMBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Sheria na Hadhi za wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku ikiwa imepitisha jina la Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kuitumikia Yanga SC kuanzia msimu huu 2016/17 baada ya kuona kuwa hana tatizo katika usajili, badala yake madai ambayo pande husika zinaweza kudaiana wakati mchezaji anaendeleza kipaji chake.
    Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote na kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan Kessy limeegemea kwenye madai na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo kuwa alianza kuitumikia Yanga kabla ya kumaliza mkataba wake Simba SC. Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016.
    Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Yanga SC wakati mchezaji huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. 
    TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.
    Kanuni hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza kwa hoja ya madai badala yake suala hilo linaweza kumalizwa wakati mashindano yanaendelea. Kamati inaendelea kupitia malalamiko na pingamizi za wachezaji wengine na inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu wachezaji wote wakati wowote kuanzia sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HII NDIYO TAARIFA RASMI YA TFF KUHUSU HASSAN KESSY NA MKATABA WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top