• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 09, 2020

  RONALDINHO ATOLEWA GEREZANI, AHAMISHIWA HOTELI YA KIFAHARI

  NYOTA wa zamani wa Barcelona na Brazil, Ronaldinho Gaucho, ametolewa gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje, lakini atakuwa kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano nchini Paraguay.
  Ronaldinho, bado anafanyiwa uchunguzi zaidi kwa kosa lake la kughushi hati ya kusafiria (Passport), ambapo machi 6 mwaka huu, yeye na kaka yake, waliingia Paraguay wakiwa na Passport bandia, zilizowatambulisha kuwa ni raia wa Paraguay.
  Wawili hao walihukumiwa miezi sita kwenda jela, lakini baada ya kuripotiwa kulipa dhamana ya Pauni milioni 1.3, wametolewa na wataendelea kutumikia kifungo cha nje.
  Ronaldinho Gaucho atakuwa kwenye hoteli ya nyota tano nchini Paraguay baada ya kutolewa gerezani PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Ronaldinho mwenye miaka 40, atakuwa akiishi kwenye chumba cha gharama zaidi katika Hotel ya nyota tano ya Palmaroga iliyopo mji mkuu wa Paraguay, Asuncion. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDINHO ATOLEWA GEREZANI, AHAMISHIWA HOTELI YA KIFAHARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top