• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 06, 2020

  MAMA YAKE GUARDIOLA AFARIKI KWA VIRUSI VYA CORONA

  KLABU ya Manchester City imethibitisha kifo cha mama wa kocha wao mkuu, Mspaniola Pep Guardiola kwa ugonjwa wa COVID 19.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamethibitisha leo kwamba Dolors Sala Carrio amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 mjini Manresa, Barcelona.
  Taarifa ya Man City imesema: "Familia ya Manchester City  inasikitika kutangaza kifo cha mama yake Pep, Dolors Sala Carrio kilichotokea leo huko Manresa, Barcelona baada ya kusumbuliwa na virusi vya corona. 

  Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola (kulia) akiwa na mama yake, Dolors Sala Carrio aliyefariki dunia leo kwa ugonjwa wa COVID 19 

  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamethibitisha leo kwamba Dolors Sala Carrio amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 mjini Manresa, Barcelona.
  Habari hizo za kusikitisha zinakuja wiki kadhaa tangu Guardiola achangie Pauni 920,000 kusaidia mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona nchini Hispania katika mfuko wa Angel Soler Daniel Foundation.  
  Mfuko huo umepewa jina la Daktari wa Santpedor ambaye alifariki duna miaka ya 1970 - mji ambao ametokea Guardiola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMA YAKE GUARDIOLA AFARIKI KWA VIRUSI VYA CORONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top