• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 12, 2020

  YANGA ILIYOANZA VIBAYA KAGAME 1999 IKATWAA KOMBE KAMPALA

  KIKOSI cha Yanga SC kabla ya mchezo wa kwanza wa Kundi D Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Rayon Sports ya Rwanda Uwanja wa Nakivubo Jijini Kampala, Uganda Januari 4 mwaka 1999. 
  Kutoka kulia waliosimama ni Kocha Msaidizi Freddy Felix Minziro, Salvatory Edward, Ally Mayay, Goliath Mwakipesile, Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu), Said Mhando (marehemu), Shaaban Ramadhani, Akida Makunda, Bakari Malima, Joseph Katuba (marehemu), Eustace Bajwala na Edibily Lunyamila. Rayon ilishinda 3-0, mabao ya Kombi Mussa dakika ya 10 kwa penalti, Ndaleni Kakule dakika ya 78 na Claude Kalisa dakika ya 9, ingawa Yanga ilizinduka na kulipa kisasi kwenye mchezo wa marudiano hadi kutwaa Kombe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA ILIYOANZA VIBAYA KAGAME 1999 IKATWAA KOMBE KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top