• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 20, 2020

  BEKI WA SIMBA SC, GARDIEL MICHAEL MBAGA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI MKOANI MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kushoto wa klabu ya Simba, Gardiel Michael Mbaga amefiwa na baba yake mzazi, Michael Mbaga Kamagi leo mjini Morogoro.
  Kwa mujibu wa taarifa ya klabu yake, baba yake amefariki mjini eneo la Bwawani mkoani Morogoro na ripoti zinasema alikuwa anaumwa.
  “Mchezaji wetu Gardiel Michael amefiwa na baba yake leo asubuhi. Tunatoa pole kwa Gardiel, familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa kuondokewa na mpendwa wao,”imesema taarifa ya klabu ya Simba leo.


  Pole Gardiel Michael Mbaga kwa kufiwa na baba mzazi. Mungu ampumzishe kwa amani mpendwa wetu. Amin.

  Michael Mbaga Kamagi leo mjini Morogoro.Gardiel yupo katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe Simba SC akitokea kwa mahasimu, Yanga SC alikodumu kwa misimu miwili baada ya kuwasili akitokea Azam FC iliyomuibua katika mfumo wake wa soka ya vijana.
  Ikumbukwe Machi 17, mwaka huu TFF ilisimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
  Pia TFF ilivunja kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizopangwa kuanza Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon ambazo pia zimeahirishwa kwa sababu ya COVID 19.
  Kwa ujumla CAF ilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kufuatia mlipuko wa virusi vya corona hadi hapo itakapaoamuliwa vinginevyo.
  Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
  Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI WA SIMBA SC, GARDIEL MICHAEL MBAGA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI MKOANI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top