• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 06, 2020

  WADAU WA KUNDI LA SPORTS VISION WAMPIGA JEKI JELLAH MTAGWA, BEKI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ANAYEUMWA KWA MUDA MREFU

  Wadau wa michezo wa kundi la Whatsapp la Sports Vision, Bakari Malima (kulia) na Mkala Fundikira (kushoto) wakimkabidhi msaada wa jumla ya Sh. 500,000 beki wa kimataifa wa zamani wa Tanzania, Jellah Mtagwa (katikati) anayesumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu walipomtembelea nyumbani kwake, Magomeni Kagera Jijini Dar es Salaam leo.

  Wanachama wa kundi la Sports Vision walijichangisha fedha hizo kwa lengo la kumsaidia Jellah Mtagwa, ambaye kama Bakari Malima (kulia) wote ni mabeki wa kati wa zamani wa Taifa Stars, klabu za Yanga SC na Pan Africans kwa vipindi tofauti. Jellah alianzia Yanga miaka ya 1970 akamalizia Pan miaka ya 1980, wakati Malima aliibukia Pan miaka ya 1990 mwanzoni akamalizia Yanga mwishoni mwa miaka hiyo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WADAU WA KUNDI LA SPORTS VISION WAMPIGA JEKI JELLAH MTAGWA, BEKI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ANAYEUMWA KWA MUDA MREFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top