• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 05, 2020

  FURY AMTAKA JOSHUA KABLA YA KURUDIANA TENA NA WILDER

  BONDIA Tyson Fury 'Gypsy King' anataka zaidi pambano la kuunganisha mataji ya dunia ya uzito wa juu dhidi ya Muingereza mwenzake, Anthony Joshua kuliko kupigana kwa mara ya tatu na Mmarekani Deontay Wilder. 
  Fury anayeshikilia taji la WBC ambaye sasa amefikisha mapambano 30 ya kushinda akiwa hajapoteza hata moja zadi ya droo kwenye pambano la kwanza na Wilider, anataka kuwa bingwa asiyepingika wa uzio wa juu duniani.
  Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa pamoja na timu yake wanajaribu kushawishi pambano dhidi ya Wilder liwekwe pembeni kwanza apiga e na Joshua, bingwa wa mataji ya WBA, WBO na IBF.

  Tyson Fury anataka zaidi pambano la kuunganisha mataji dhidi ya Anthony Joshua kuliko kupigana tena na Deontay Wilder PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Waingereza hao wote tayari wana ratiba ya mapambano yajayo - Fury dhidi ya Wilder na Joshua dhidi ya Kubrat Pulev Uwanja wa Tottenham Hotspur.
  Pambano kati ya Joshua na Pulev lilipangwa kufanyika Juni 20 Kaskazini mwa London na sasa limesogezwa mbele hadi Julai 25 kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona duniani kote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FURY AMTAKA JOSHUA KABLA YA KURUDIANA TENA NA WILDER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top