• HABARI MPYA

  Sunday, April 19, 2020

  STARS ILIYOIPIGA HARAMBEE 3-1 NA KUTWAA KOMBE LA CASTLE 2001

  KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifs Stars kabla ya mchezo wa fainali ya Kombe le CECAFA Castle Oktoba 27, mwaka 2001 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Kutoka kulia waliosimama Kocha Msaidizi, Charles Bonphace Mkwasa, Daktari Ramadhani Mkuna na wachezaji, Waziri Mahadhi, Nteze John, Boniphace Pawasa, Mecky Mexime, John Mwansasu na Kocha Mkuu, Syllersaid Mziray (marehemu). Waliochuchumaa kutoka kulia ni Yussuf Macho, Joseph Kaniki, Salvatory Edward, Alphonce Modest, Said Maulid na Manyika Peter.  Tanzania ilishinda 3-1, mabao yake yakifungwa na Yussuf Macho dakika ya 26, Emmanuel Gabriel aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kaniki dakika ya 66 na Salvatory Edward dakika ya 90, wakati la Kenya lilifungwa na Robert Mambo dakika ya 85.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ntambadila wa Ntambadila kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Waziri Mahadhi alishindwa kuendelea baada ya dakika 10 tu kufuatia kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Suleiman Matola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS ILIYOIPIGA HARAMBEE 3-1 NA KUTWAA KOMBE LA CASTLE 2001 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top