• HABARI MPYA

  Saturday, April 04, 2020

  KOCHA WA AZAM FC ASEMA WACHEZAJI WAKE WAPO KATIKA WAKATI, LAKINI HAKUNA NAMNA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kwamba anafahamu wachezaji wake wapo katika wakati mgumu kufuatia klabu kusitisha maozezi ya pamoja kutoka na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID19).
  “Najua ni wakati mgumu kwa wachezaji, wanataka kufanya mazoezi na kucheza, sio kukaa nyumbani, lakini wakati huu unahitaji kutuunganisha na kuwa na nguvu zaidi katika siku zijazo. Nawatakia kila mtu Tanzania na mashabiki wa Azam afya njema," amesema Cioaba.
  Kocha huyo raia wa Romania, amekuwa akitoa programu za mazoezi binafsi kwa wachezaji katika kupindi hiki walichokuwa nyumbani kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa wa virusi vya CORONA (COVID - 19).
  “Nadhani ni muhimu kwamba katika wakati huu mgumu tunaopitia kuonyesha umoja, mshikamano na uelewa," alisema. 
  Machi 17, mwaka huu TFF ilisimamisha Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na mashindano yake mengine yote, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona duniani kote.  
  Ligi Kuu ilisimama huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa pointi zake 71, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 54 baada ya timu zote kucheza mechi 28, wakati vigogo, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 51 za mechi 27 na Namungo wa nne wakiwa na pointi 50 za mechi 28.
  Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa pointi zake 15 za mechi 29, nyuma ya Mbao FC pointi 22 mechi 28, Alliance FC pointi 29, mechi 29, Mbeya City pointi 30 mechi 29 na Ndanda FC pointi 31 mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA AZAM FC ASEMA WACHEZAJI WAKE WAPO KATIKA WAKATI, LAKINI HAKUNA NAMNA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top