• HABARI MPYA

  Wednesday, April 08, 2020

  MECHI ZILIZOSALIA SERIE A KUMALIZIWA ROMA BILA MASHABIKI

  UONGOZI Serie A nchini Italia unafikiria uwezekano wa kumalizia mechi zote 12 za ligi hiyo zilizosalia katika Jiji la Roma kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19.
  Kwa mujibu wa gazeti la La Repubblicachama cha soka nchini Italia, kinatafakari kwa kina namna ya kumalizia msimu huu, huku wakipata wazo hilo la kucheza michezo sehemu moja, jambo ambalo halijawahi kufanyika.
  Kama ilivyo kwa Ligi zote na mashindano mbalimbali duniani, Serie ilisitishwa katikati ya mwezi uliopita kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.

  Serie A inafikiria kumalizia mechi zote 12 za ligi hiyo zilizosalia katika Jiji la Roma kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona 

  Klabu zote 20 za Serie A zitakwenda Rome kumalizia msimu huu kwa muda wa siku 45, yaani mwezi mmoja na nusu kwenye mechi ambazo mashabiki hawataruhusiwa kuingia uwanjani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZILIZOSALIA SERIE A KUMALIZIWA ROMA BILA MASHABIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top