• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2020

    KLABU KUBWA NCHINI ZINAZIDIWA MAARIFA NA WASANII MAARUFU

    Na Ally Kamwe, DAR ES SALAAM
    UKIPITIA ripoti ya mwaka ya mapato ya klabu nyingi duniani, utaona zinategemea vyanzo vikuu vitatu vya mapato, ambavyo ni Haki za Matangazo ya Televisheni, Mauzo ya bidhaa za klabu na Mapato ya Viingilio vya mechi.
    Wakati huu Ligi zikiwa zimesimama kwa sababu ya janga la maambukizi vya virusi vya corona au COVID 18, baadhi ya Klabu zimeanza kutetereka kiuchumi
    Kwanini? Jibu ni rahisi sana. Vyanzo vyao vya mapato vimeathirika na virusi vya Corona. Mechi hazionyeshwi, mauzo ya bidhaa za klabu yameshuka, hakuna pato la viingilio.
    Nguvu pekee iliyosalia ni fedha za wadhamini. Wenye Brand kubwa, wananufaika na madili makubwa waliyosaini.
    Je, umeshawahi kujiuliza, Ni njia gani timu inaweza kuendelea kuzalisha mapato hasa katika kipindi hiki? 
    Kuna fursa ya dhahabu kupitia DIGITAL PLATFOM za klabu ( Website, YouTube,  App, Instagram, Twitter na Facebook).
    Ngoja nikwambie kitu, Februari 20, 2017, Manchestee United ilimwajiri Phil Lynch kama CEO wa kitengo cha MEDIA.
    Kabla ya ajira hiyo, Lynch alishawahi kufanya kazi katika kampuni ya Yahoo na Sony Pictures. Miongoni mwa Kampuni kubwa sana duniani.
    Kazi yake kubwa pale Old Trafford ilikuwa ni kutafuta jinsi gani Man United itatengeneza fedha zaidi kupitia mitandao
    Kitu cha kwanza Lynch alichokifanya kwenye kazi yake ni kutofautisha kati ya FANS na FOLLOWERS.
    Cha pili ilikuwa ni kufanya tafiti ya kujua ni tofauti ya umri gani unaofatilia mitandao yao? Wakati gani wanasomwa/kutazamwa sana, content zipi zinauza, na wana wafuasi sana maeneo gani duniani.
    Ajabu ni kuwa, TANZANIA inashika nafasi ya 4 katika zile 5 a juu zinazoongoza kufatilia habari za Manchester United kupitia mitandao.
    Lengo langu si kutaka kukuonyesha jinsi United wanavyofanya kazi, lengo ni kutaka kukuhabarisha kuwa IDARA HII YA HABARI ya United inachangia  11% ya pato la Timu kwa mwaka. 
    Na kipindi hiki ambacho, matumizi ya mitandao yameongezeka, inatajwa United Idara hii itachangia kwa 17%. 
    Nirudi kwenye hoja, juzi na jana, mmekuwa mkinitajia wapiga picha bora wa Klabu zetu za VPL
    Jambo zuri zaidi, Wakuu wa Idara za klabu za Azam FC, Simba SC walishiriki kutaja vijana wao
    Kaka yangu Dismas TEN nae akamtaja kijana wake Chicharito, kama mpiga picha bora. Ni kweli, vilabu vyetu vina wapiga picha bora, lakini tumeshawahi kujiuliza kama kweli KLABU ZETU zina vitengo bora vya Habari?
    Tunawatumiaje hawa wapiga picha bora tulionao kutengeneza pato la klabu?
    Simba wako active sana Instagram. Lakini YouTube kwenye hela iliyonyooka, wanadorora. Hawako active
    Azam pia. Wanaposti kwa kusuasua. Yanga ndio aibu. Klabu kubwa mpaka leo haina akaunti ya Youtube iliyo active.
    Wasanii wa Kitanzania wanaingiza fedha nyingi sana kwa mwezi kupitia biashara ya mitandao. Inawezekana vipi klabu yenye mashabiki zaidi ya Milioni 10 iwe na mapato SEFURI kwenye biashara ya mtandao? Kuna kitu hakiko sawa.
    Vita imekuwa ni kugombea Followers ambao tunashindwa kujua thamani yao katika jicho la kibiashara.
    Nafikiri umefika wakati sasa, Viongozi na Mashabiki kuanza kuwahoji Wakuu wao wa vitengo vya habari, MNA FAIDA GANI KWA TIMU YETU?
    (Ally Kamwe ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa Azam TV, unaweza kumfollow @allykamwe)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLABU KUBWA NCHINI ZINAZIDIWA MAARIFA NA WASANII MAARUFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top