• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 01, 2020

  LIGI YA MABINGWA NA EUROPA LEAGUE ZASOGEZWA HADI AGOSTI

  HATUA zijazo za michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League zimeripotiwa kusogezwa hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona linaloendelea duniani kote. 
  Mechi zote za timu za taifa zilizopangwa kuchezwa Juni zimeahirishwa ili kuupisha msimu wa 2019-20 ukamilishwe.
  Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) baada ya mkutano uliofanyka kwa video leo. 
  Mechi, mashindano na ligi zote za soka Ulaya zimesitishwa tangu katikati ya Machi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, ulioanzia Wuhan huko China mwishoni mwa mwaka jana.

  Michuano ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League imesogezwa mbele hadi Julai na Agosti kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA NA EUROPA LEAGUE ZASOGEZWA HADI AGOSTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top