• HABARI MPYA

  Sunday, April 19, 2020

  SAFARI NGUMU ZA WAAFRIKA KATIKA KUTIMIZA NDOTO ZAO KWENYE SOKA

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  WAKATI dunia ikiibatiza Afrika na nchi zake kuwa sehemu ya dunia ya tatu, dunia ambayo maisha ya mwanadamu wa wa kawaida katika bara hili yakiwa na changamoto lukuki zinazofanya ndoto nyingi za vijana wa bara hili kuishia njiani au kutimia kwa shida kweli kweli.
  Waafrika hupitia njia  nyingi shida, vikwazo, hila na kila aina ya changamoto katika kutimiza ndoto zao.
  Katika ramani ya soka vijana wengi wakiafrika huathiriwa na changamoto hizi katika kutimiza ndoto zao na kuifikia edeni ya mafanikio,  wengi wenye asili ya bara hii hupata ahueni ya safari hii pale tu wanapokuwa wamezaliwa na kukulia ng'ambo au la kuhamia ng'ambo wakiwa katika umri mdogo.

  Licha ya changamoto ya umaskini mkubwa na wakutupwa unaotesa familia nyingi za kiafrika, umaskini wa nchi uliozaa uhaba wa miondombinu, athari za kisiasa na vita za wenyewe kwa wenyewe pia zinazidi kupigilia msumari wa moto safari za utimizaji ndoto kwa vijana wengi wa bara hili..
  Hivi ushawahi sikia story ya Sadio Mane?, wakati Pierre Emerick Augbameyang akizaliwa na kukulia Spain, Sadio Mane amekulia huko kijijini katika mji wa Sedhiou nchini Senegal katika familia yenye rundo la umaskini, sio viatu tu vilikuwa shida kwa Saido Mane kwani mpaka bukta ya kuchezea kwake ilikuwa msala kuipata hali iliyomfanya afanye majaribio yake ya kwanza mbele ya macho ya mawakala waliozamia kijijini kwao akiwa na bukta iliyochanika vibaya na kuacha bahadhi ya maeneo yake muhimu ya mwili  yakiwa wazi  huku viatu alivyovaa vikiwa katika hali mbaya zaidi tena bado vikiwa si vyake ni vya kuazima.
  Yes..! Ni yeye!! Sadio Mane huyu ambaye sasa anaimbwa kila weekend katika majukwaa yote pale Anfield...Sadio mlMane huyu pamoja na Janga la   Corona bado pale Madrid   wanawaza nini wafanye ili atue katika klabu yao.
  Story ya Sadio Mane inabeba taswira halisi ya njia wanazopita nyota wengi wakiafrika katika safari yao kisoka, kuanzia Younde, Douala Cameron, pwani ya Aivori, Gambia, Guinnea, Angola mpaka kwetu afrika ya mashariki na kusini.
  Safari za akina Yaya Toure na ndugu yake Tolo Toure zilijaa changamoto isiyoelezeka, vipi kuhusu wale watoto wa Accra?
  Ushawahi sikia story ya Lamptey kuendesha baiskeli kutoka Ghana mpaka Nigeria kutafuta nafasi ya kutimiza ndoto zake kisoka? Ushawahi sikia story za watoto wa Nigeria wanavyohangaika kule makoko kucheza soka? Huko ndiko akina jay jay okocha, taribo west na wengine wengi waliposotea ndoto zao, huko ndiko wale vijana walipoamua kudanganya umri ili mradi tu watimize ndoto zao.
  Ni changamoto hizo wanazopitia waafrica katika kutimiza ndoto zao kisoka,  wakati harry Kane akianzia soka lake katika academy toka akiwa na miaka 5, kijana wakiafrica pale goma nchini DRC anahangaika kuyaokoa maisha yake dhidi ya waasi wa msituni, kijana mwengine anakimbiza uhai wake kule Mogadishu dhidi ya alshababi, soka wanalicheza kwenye ardhi yenye shida, milio ya risasi, mabomu nk, bila ya viatu huku mpira ukiwa haujulikani hata kampuni iliyoyengenezwa kwa kuchakaa kwake, huko ndiko walikotoka akina romana lualua yule mwamba wa DRC, ndio huko yule mwanaume nonda shabani aliyewanyesha real Madrid ya zidane na delima uefa 2004 akiwa na as monaco, hakikuwa rahisi kwa nonda hata kidogo, haikuwa rahisi kwa okocha na wala haikuwa rahisi kwa yaya Toure.
  Hakuna masika yasiyo na mbu wahenga walisema, lakini safari za vijana hawa wakiafrica mbu wake wamezidi kweli kweli na kutishia sana utimilishwaji wa ndoto zao kisoka, ukiwaza juu ya changamoto zakisoka walizonazo vijana wajuba kule sudani kusini unakaa chini na kuipitia safari ya sadio berahino na ukimbizi wake kule uingereza, wakati unawaza alichofanya Michael Olunga kutimiza ndoto yake, vuta picha zile purukushani alizokutana nazo mtoto wa mbagala na shujaa watanzania Mbwana Ally Sammata, kucheza kwenye viwanja vyenye uzio wamabati yenye tishio la mbwa mkali, kisha kutembea kwa miguu kutoka mbagala zakhem mpaka uwanja wa mabatini ulioko tandika kwenda kucheza mechi moja ya ndondo.
  Hii ndio Afrika na changamoto zake, ndiyoo!!Tunafika lakini changamoto zake ni kubwa kuliko!
  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya instagram kama @dominicksalamba au nambari ya simu)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAFARI NGUMU ZA WAAFRIKA KATIKA KUTIMIZA NDOTO ZAO KWENYE SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top