• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 11, 2020

  SVEN LUDWIG VANDENBROECK ASEMA ANAFURAHIA USHIRIKIANO NA WASAIDIZI WAKE SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya wa Simba SC, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amesema anafurahia ushirikiano na Wasaidizi wake na anaamini utaleta mafanikio makubwa klabu.
  Lakini Vandenbroeck amesema kwamba haikuwa kazi nyepesi kwake kuendana na wasaidizi wake hao, kwani mwanzoni ilimuwia vigumu kidogo.
  “Mwanzoni kufanya nao kazi haikuwa rahisi, lakini ukiliangalia sasa utaona tunashirikiana sana na hata ukiangalia moja ya picha iliyopigwa na mtu wetu wa habari utaona kwamba kila kitu kinafanyika vizuri.” Amesema Vandenbroeck mwenye umri wa miaka 40 tu.
  Vandenbroeck anasaidiwa na wazalendo Suleiman Matola (Msaidizi Namba Moja), Muharami Mohamed ‘Shilton’ (Kocha wa makipa) na Mtunisia, Adel Zrane (Kocha wa Fiziki).
  Benchi la Ufundi la Simba SC linakamilishwa na Daktari Mkuu, mzawa pia Yassin Gembe na Mtaalamu wa Tiba ya Viungo, Mjerumani Paulo Gomez Dardenne.
  Vanderbroeck, alijiunga na na Simba SC Desembna 12 mwaka jana baada ya kuachana na timu ya taifa ya Zambia, akichukua nafas ya Mbelgiji mwenzake Patrick Aussems aliyefukuzwa.
  Hadi sasa, Sven Ludwig Vandenbroeck ameiongoza Simba SC katika mechi 24, ikishinda 20, kufungwa tatu, zote 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar, JKT Tanzania na watani wao wa jadi, Yanga katika Ligi Kuu. Ilitoa sare moja, 2-2 na Yanga katka Ligi Kuu pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SVEN LUDWIG VANDENBROECK ASEMA ANAFURAHIA USHIRIKIANO NA WASAIDIZI WAKE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top