• HABARI MPYA

    Tuesday, February 07, 2017

    AIRTEL, TFF WAUNGANA KUIPIGIA KAMPENI SERENGETI BOYS

    Na Mwandkishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya simu ya Airtel sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamewataka wadau kujitokeza kuisapoti timu ya vijana ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys baada ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika za U-17 nchini Gabon Mei mwaka huu.
    Malinzi na Airtel wasema hayo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana.
    Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akifafanua jambo. Kushoto ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo, Ayoub Nyenzi 

    Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa.
    Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando amesema kuwa wanawapongeza TFF kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuifikisha hapa Serengeti Boys ila bado vijana hawa wanahitaji kupata sapoti kutoka kwa wadau na seriakali kwa ujumla.
    Mmbando amesema kuwa,  vijana hawa wanahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi na kujengwa kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwani waliona walishaondolewa  kwenye michuano hiyo.
    "Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili waweze kufanikisha safari yao ya Gabon mwezi wa tano na sisi kama airtel tutasaidia katika kuitangaza timu hiyo,"amesema Mmbando
    Airtel wamekuwa wadau wakubwa sana wa kukuza soka la vijana kwa kuanzisha mashindano ya Airtel Rising Star ambapo hivi karibuni waliweza kufanya usaili wa vijana na wengine wakiwa tayari kwenye kikosi cha vijana wa Serengeti Boys.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AIRTEL, TFF WAUNGANA KUIPIGIA KAMPENI SERENGETI BOYS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top