• HABARI MPYA

    Monday, March 04, 2013

    TFF WAIPONGEZA AZAM NA KUITAHADHARISHA BODI YAKE

    Azan oyee

    Na Boniface Wambura
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeipongeza klabu ya Azam ya Tanzania Bara kwa kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, CAF.
    Taarifa ya TFF, imesema kwamba ushindi wa jumla ya mabao 8-1 ambao Azam imeupata dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini si fahari kwa timu hiyo tu, bali Tanzania kwa ujumla, na unaonyesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kiushindani katika michuano hiyo ya Afrika.
    Hata hivyo, TFF imesema ni vizuri Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo wakautazama ushindi huo kama changamoto kwao kuhakikisha wanajipanga vizuri zaidi kwa raundi inayofuata.
    Timu ya Azam inayofundishwa na Mwingereza John Stewart Hall ilishinda nyumbani mechi ya kwanza mabao 3-1, na jana kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 ugenini jijini Juba.
    Kwa kufanikiwa kuing’oa Al Nasir Juba, Azam sasa watacheza raundi ya kwanza (raundi ya 16 bora) ya michuano dhidi ya Barrack Y.C.II ya Liberia ambayo katika raundi ya awali iliitoa Johansens ya Sierra Leone. 
    Barrack ilishinda bao 1-0 nyumbani katika mechi ya kwanza na kulazimisha suluhu katika mechi ya marudiano jijini Freetown.
    Azam itaanzia mechi hiyo ugenini kati ya Machi 15,16 na 17 mwaka huu wakati mechi ya marudiano itachezwa Tanzania kati ya Aprili 5,6 na 7 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TFF WAIPONGEZA AZAM NA KUITAHADHARISHA BODI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top