• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 21, 2013

  WENGER KUHAKIKISHIWA MAISHA EMIRATES NA KIKAO CHA BODI PAMOJA NA KUJAZWA FEDHA ZA KUSAJILI


  ARSENE Wenger atahakikishiwa kuwa mtu sahihi wa kuifufua Arsenal, wakati wa Mkutano wa Bodi utakaomuhusisha Mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke, Leo.
  Klabu hiyo imethibitisha kuwa Wenger atakutana na Kroenke, ambaye alikuwa London kuishuhudia klabu yake ikipigwa kwa mabao 3-1 na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa Juzi.
  Tumaini pekee la ubingwa la Arsenal msimu huu ni kwenye Ligi ya Mabingwa na wanatakiwa kujitahidi kubadili matokeo kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Munich, Machi 13 na wanataka kuhakikisha wanapata nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya England.

  Under pressure: Arsene Wenger saw Arsenal crash out of the FA Cup and go 3-1 behind to Bayern Munich in the Champions League
  Shakani: Arsene Wenger aliishuhudia Arsenal, ikitolewa kwenye Kombe la FA, na mpaka sasa wako nyuma ya Bayern kwa mabao 3-1, Ulaya.

  Time to talk: Arsenal owner Stan Kroenke is set to speak with Wenger
  Tuongee: Mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke anajipanga kuongea na Wenger
  The Gunners, ambao wanakamata nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu, wanakutana na Aston Villa, Emirates, Jumamosi, katika mechi muhimu ambayo ni lazima washinde ilikuzima hasira za mashabiki.
  Wenger, anawakati mgumu kwa sasa hasa baada ya kukaa miaka nane bila ubingwa, anajiandaa kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake, mwisho wa msimu huu.
  Lakini, licha ya mashabiki kutokuwa na imani naye, hayuko kwenye hatari ya kutimuliwa na bodi ya klabu huku mkataba wake ukifika tamati 2014.
  Wenger alishitushwa na tofauti kubwa iliyopo kati ya kiwango cha timu yake na Bayern, lakini atajulishwa kama kuna fedha kibao za kutumia wakati wa usajili. Kushindwa kumaliza kati ya timu nne za juu kwenye ligi kunaweza kuharibu mipango yake, na kama wakishindwa kumaliza katika nafasi hizo hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufanya hivyo tangu Wenger alipojiunga nayo mwaka1996.
  Arsenal wanakiasi cha pauni milioni 150, mkononi, na hizo zinaweza kuanza kutumika pale mkataba wa miaka mitano kati ya klabu hiyo na mdhamini wa vifaa Emirates utakapoanza wakati wa majira ya joto.
  The Gunners pia wamekuwa kwenye majadiliano na watengenezaji wa vifaa vya michezo Nike, juu ya haki ya upekee, lakini adidas wametokea kutoa upinzani mkubwa sana. Japokuwa fedha za mkataba mpya bado hazijatangaza hadharani, hizo pia zitakuwa kwa ajili ya Wenger.
  Kocha huyo anawatolea macho mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic, Kipa wa Liverpool, Pepe Reina, Mario Gotze wa Borussia Dortmund , Victor Wanyama wa Celtic na Etienne Capoue wa Toulouse.

  Dejected: Arsenal's players look disappointed after being defeated by Bayern
  Huzuni: wachezaji wa Arsenal wakionekana wenye huzuni baada ya kufungwa na Bayern

  Wenger ataongea na msaka vipaji mkuu wa klabu hiyo Steve Rowley na wasaka vipaji wengine, na kujadili juu ya mipango ya kiangazi. Imefahamika kwamba wanafanya kazi ya kuangalia wachezaji sawia kwa klabu hiyo, huku wakijua wazi kuwa kuna suala la kupunguza matumizi.
  Pia kuna dalili ndogo sana kwa wachezaji ambao Wenger anawatolea macho kukubali kujiunga na timu hiyo kama haitakuwa inashiriki mchuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini Wenger bado anaungwa mkono na wachezaji na Bodi, licha ya kufanya vibaya.


  Mario Gotze
  Pepe Reina
  Wanatakiwa: Mario Gotze na Pepe Reina wako kwenye rada za Wenger.

  Nahodha Thomas Vermaelen alisema: “Nimeshangazwa na watu wanaomlaumu Kocha. Kila mtu kwenye soka anaangalia mipango ya muda mfupi. Haimaanishi kwamba mambo yakiwa mabaya kwa sasa ndiyo tunamtenga kocha. Ni mtu sahihi na tuko nyuma yake, tunatakiwa kuonyesha hilo uwanjani.”
  Theo Walcott alikubaliana na hilo, akisema: “Tuna mtu sahihi wa kuturudisha kwenye mafanikio.”
  Wakati huo huo, washauri wa Bacary Sagna wanaangalia uwezekano wa kumpeleka Paris St-Germain. Mfaransa huyo anamatatizo yake binafsi kwenye klabu hiyo na kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka mwisho wa msimu huu, tayari watu wa Arsenal wanatafuta mtu wa kurithi nafasi yake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WENGER KUHAKIKISHIWA MAISHA EMIRATES NA KIKAO CHA BODI PAMOJA NA KUJAZWA FEDHA ZA KUSAJILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top