• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 21, 2013

  GLENN MURRAY NDIYE ANAYEMFUATIA MESSI KWA KUFUNGA MABAO DUNIANI

  BIN ZUBEIRY imetambua kwamba Glenn Murray yuko nyuma ya Lionel Messi katika orodha za wafungaji kwenye ligi zote msimu huu.
  Baada ya kuangalia madaraja mawili ya juu Ulaya kwenye ligi tano bora za Ulaya tumegundua ni Messi pekee ambaye amempita mshambuliaji hatari wa  Crystal Palace kwa mabao msimu huu.
  Akifunga bao la kwanza kwenye mechi ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Bristol City, usiku wa Jana, Murray alifikisha mabao 28 msimu huu.

  Angalia video...
  Goal machine: With Cardiff City slipping up last night Murray's goal helped close the gap on the leaders
  Mashine ya Mabao: wakati Cardiff City wakiteleza jana usiku,bao la Murray  liliisaidia Palace kuisogelea Cardiff

  Murray ni zao jipya kutoka Spotland 

  Kutakuwa na kitu kwenye maji ya Spotland, kwa  Rochdale kufanikiwa kuzalisha washambuliaji hatari siku za karibuni.
  Mashabiki wa Ligi Kuu ya England, watakuwa wanawajua kina Grant Holt na Rickie Lambert – ambao walicheza pamoja Dale katika msimu wa 2005-06, chni ya Steve Parkin – lakini walisajiliwa kuwarithi waliopoondoka kwenda Nottingham Forest na Bristol Rovers hawakuwa wabaya pia.
  Adam Le Fondre, ambaye kwa sasa anachezea Reading, pamoja na mfungaji bora Ligi Daraja la Kwanza akiwa na Crystal Palace, Glenn Murray walisajiliwa kuziba nafasi hizo.
  Murray – ambaye alifunga mabao 25, kwenye mechi 58 akiwa na Rochdale – Jana amefunga bao dhidi ya Bristol City na kufikisha mabao 28 msimu huu.
  Akiwa na miaka 29, Murray siyo mchezaji wa msimu, lakini kama anataka kupata moyo zaidi na kujiamini kwamba anastahili kucheza ligi za juu anatakiwa kuangalia wachezaji wenzake waliowahi kupita Spotland.
  Holt na Lambert wameonyesha ubora wao kwenye vikosi vya Norwich na Southampton msimu huu.
  Akili ya Murray na uwezo wake wa mipira ya juu, inamfanya kuwa hatari zaidi kwa mabaeki na kama Palace wataendeleza kasi yao hiyo basi kuna nafasi kubwa kwa mchezaji huyo kuungana na wenzake kutoka Rochdale kwenye Ligi Kuu
  ndful for any defender, and if Palace continue the way they are going then he will be joining the strong ex-Rochdale contingent in the Premier League before too long. Joe Ridge

  Murray kwa kiasi kikubwa amekosa umaarufu kutokana na kufunikwa na Wilfred Zaha ambaye ametua Manchester United, kwa ada ya pauni milioni 15.
  Lakini Murray ambaye kwa sasa ndiye mfungaji bora nchini England akiwa mbele ya Tom Pope wa Port Vale kwa mabao matatu na mabao saba zaidi ya Robin van Persie wa Man United.
  Mabao yake yamemfanya akamate nafasi ya pili kwa ufungaji, nyuma ya Messi ambaye juzi alifunga bao lake la 301 akiwa na miamba ya Catalan.
  Cha kushangaza Ligi Daraja la Kwanza inaongoza kwa ufungaji kwenye ligi za madaraja ya chini huku Murray, Charlie Austin, Jordan Rhodes na Matej Vydra wakishika nafasi nne za Juu, nafasi ya tano ndiyo inashikiliwa na Marco Sansovini wa Serie B, akiwa na mabao 18.
  Wakati ambao mpinzani wake Muargentina amefunga mabao 37, kwenye mechi 24 za La Liga msimu huu na wazi kwa, Murray anakazi kubwa sana ya kumfukuzia.
  Lakini akili yake yote itakuwa kuhakikisha anaipandisha timu yake msimu huu.
  Mzaliwa huyo wa Cumbria, Murray alianza kucheza asoka kwenye klabu ya mtaani ya Workington Reds mwaka 2002, akifunga mabao 25 kwenye mechi 43 alizocheza kwa miaka miwili.
  Alihamia Carolina Kaskazini kuchezea klabu ya Wilmington Hammerheads ambako alicheza mechi 14 tu, kabla ya kurudi England na kutua Barrow mwaka 2004.
  Murray alifunga mabao tisa katika mechi tisa  na klabu hiyo, kiwango chake kilimpeleka Carlisle – ikiwa ni klabu yake ya nne japokuwa alikuw ana miaka 21 tu.
  Baada ya kuisadia klabu hiyo kuchukua mataji mawili mfululizo mwaka 2005 na 2006, alijikuta akiwa hana nafasi kwenye klabu hiyo, na akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Stockport County na baadaye Rochdale.
  Akiwa na Rochdale Murray alifanya vizuri sana na kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu, na alikuwa na wastani wa kufunga bao moja katika kila mechi mbili.
  Alisajiliwa kwa pauni 300,000 na klabu ya Brighton mwaka 2008 na Murray alipata taji la Ligi one akiwa na klabu hiyo.
  Murray alikataa kuongeza mkataba mpya baada ya kudumu na klabu hiyo kwa miaka mitatu, na kutua Crystal Palace.


  Top of the shots: Europe's No 1 goalscorer Lionel Messi has been in phenomenal form for Barcelona
  Kiongozi: Mfungaji bora wa Ulaya Lionel Messi 
  Europe's top marksmen
  Top-flight goalscorers with minutes per goal
  Orodha: Orodha ya wafungaji Bora kwenye ligi mbalimbali za Ulaya
  Former foe: Murray used to play for Palace's biggest rivals Brighton, who are also hunting promotion
  Murray kazini wakati akiwa na klabu ya Brighton.
  Heading for victory: Murray played his part in Palace's League Cup win over Manchester United last season
  Murray alihusika kwenye ushindi wa Kombe la Ligi dhidi ya Manchester United msimu ulipopita

  Alifunga bao la ushindi lililoitupa nje ya michuano ya Kombe la Ligi Man United mwaka jana, Old Trafford.
  Licha ya kufunga mabao saba kwenye mechi 44, kocha wake pale Selhurst Park alikuwa akimuamini bado
  Imani yao kwake imejilipa, msimu huu baada ya Murray kuibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji tishio zaidi kwenye Ligi Daraja la Kwanza England.
  Na mabao 28 katika mechi 30 yamekuwa muhimu kwa klabu yake kuendelea kuifukuzia Cardiff kwenye harakati za kupanda daraja msimu ujao.

  VIDEO: Angalia shughuli ya mshambuliaji huyo dhidi ya Middlesbrough...
   VIDEO: Watch Murray score a 20-minute hat-trick as Crystal Palace come back to win after being 2-0 down at home to Cardiff...


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: GLENN MURRAY NDIYE ANAYEMFUATIA MESSI KWA KUFUNGA MABAO DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top