• HABARI MPYA

    Wednesday, February 27, 2013

    ARSENAL KUWEKA SANAMU LA DENNIS BERGKAMP NJE YA UWANJA, ATAKUWA GWIJI MWINGINE WA KLABU


    ARSENAL wanataka kuweka sanamu la Dennis Bergkamp nje ya uwanja wake, wakati wa majira ya joto, hii ikiwa alama ya gwiji mwingine wa timu hiyo.
    Sportmail limeona picha zinazoonyesha jinsi sanamu hilo litakavyo kuwa linafanana – litakuwa kwenye muundo kama wa kwenye picha ambayo alipigwa akimiliki mpira mwaka 2003 kwenye pambano dhidi ya Newcastle.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uholanzi atashuhudia sanamu lake liliwekwa pembani ya sanamu la Thierry Henry, Tony Adams na Herbert Chapman ambayo yaliwekwa Disemba mwaka jana.

    VIDEO: Angalia mabao bora ya Bergkamp akiwa na jezi ya Arsenal...
    Golden boy: The statue is based on this pose by Dennis Bergkamp controlling the ball at Newcastle
    Mwana wa Dhahabu: Sanamu hilo litafanana na picha hii ya Dennis Bergkamp akimiliki mpira dhidi ya Newcastle

    Kwa nini ni Gwiji wa Arsenal...

    Mataji matatu ya Ligi Kuu ya England
    Mataji manne ya Kombe la FA
    Mabao 87, kwenye mechi 315
    Bergkamp alikuwa kipenzi cha mashabiki wa the Gunners wakati akiwa na klabu hiyo kwa miaka 11
    Baada ya kusajiliwa na Bruce Rioch kutoka Inter Milan kwa ada ya pauni milioni 7.5 mwaka 1995, aliiongoza Arsenal kwenye kilele chake cha mafanikio na kuchukua mataji.
    Mshambuliaji huyo aliisaidia Arsenal kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England – alikuwa kwenye kikosi kilichocheza mechi 49 za ligi kuu bila kufungwa mwaka 2004 – pia alishinda mataji manne ya Kombe la FA.

    Dutch master: Bergkamp scores one of his 87 goals for Arsenal
    Mtaalamu wa Kiholanzi: Bergkamp akifunga bao lake la 87 akiwa na Arsenal
    Winning mentality: Bergkamp (second left) celebrates the 2005 FA Cup win - Arsenal's last trophy
    Akili ya ushindi: Bergkamp (wapili kushoto) akishangilia taji la FA mwaka 2005- lilikuwa taji la mwisho la Arsenal

    Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA na Waandishi wa Habari za michezo mwaka 1998.
    Msemaji wa Arsenal alisema: “Tuna masanamu matatu nje ya uwanja wa Emirates kwa ajili ya kumbukumbu ya magwiji wa Arsenal - Herbert Chapman, Tony Adams na Thierry Henry na tunashukuru kwamba yamekuwa yakiwavutia sana wanaotembelea uwanja huu.

    In charge: Bergkamp is currently working as No 2 to Ajax manager Frank De Boer
    Kazini: Bergkamp kwa sasa ni kocha msadizi wa Ajax akifanya kazi chini ya Frank De Boer

    “Tunafurahishwa na uvumi uliozagaa juu ya sanamu letu linalokuja hapa Emirates, watu wanavutiwa na taarifa hizi na tutatangaza kila kitu juu ya maendeleo ya sanamu hilo.”
    Bergkamp sasa hivi anafanya kazi kama msaidizi wa Frank de Boer katika klabu ya Ajax, baada ya kujifunza kazi hiyo kwenye klabu hiyo iliyomkuza.
    Wakati huu ambao Arsene Wenger – ambaye alimfundisha Bergkamp Arsenal kwenye miaka ya nyuma akiwa kwenye wakati mgumu ndani ya Emirates, watu wamekuwa wakitamanio kumona Mholanzi huyo akirejea klabuni hapo kama kocha.
    Wakati Liam Brady akiachia ngazi kama kocha wa chuo cha soka cha klabu hiyo, Bergkamp anatajwa kurithi jukumu hilo, lakini mwenyewe angependa kazi ya ukocha kamili wa klabu hiyo.

    Legend No 1: Thierry Henry was in tears when Arsenal unveiled his statue
    Legend No 1: Thierry Henry was in tears when Arsenal unveiled his statue
    Gwiji Namba 1: Thierry Henry alitoa machozi pale Arsenal alipoona sanamu lake kwa mara ya kwanza Disemba 2011
    Legend No 3: Herbert Chapman is the only manager with his own Arsenal statue
    Legend No 2: Tony Adams' famous pose was immortalised
    Gwiji No 2 na 3: Herbert Chapman (kushoto) na Tony Adams pia wanamasanamu yao
    Leader and legend: Tony Adams' famous celebration against Everton was captured
    Gwiji wa Magwiji: Staili ya ushanguliaji ya Tony Adams dhidi ya Everton ilitumika kwenye sanamu lake

    VIDEO: Mabao matano bora ya Bergkamp Arsenal...

    Siyo ajabu kuona Dennis Bergkamp akipata sanamu ndani ya Arsenal, hasa ukifikiria ubora wa magoli yake. 
    5: Arsenal v Southampton - Septemba 23, 1995
    Bao la kwanza la Bergkamp akiwa na jezi za Arsenal halikuwa baya kwa kuanza nalo. Akiwa ametua kutoka Inter kwa ada iliyoweka rekodi ya klabu ya pauni milioni 7.5, watau walikuwa wakitarajia makubwa kutoka kwake, hakufunga kwenye mechi zake nane za kwanza, lakini mabao yake mawili dhidi ya Southampton yalikuwa ishara tosha ya kila anachoweza kukifanya. Alifunga kwa shuti kali la moja kwa moja katika dakika ya 17 ya mchezo akimalizia krosi ya Glenn Helder shuti ambalo lilimshinda Dave Beasant. Jinsi alivyouotea mpira huo ilikuwa nzuri sana, kipindi cha pili alifunga bao lake la pili kwa shuti kali la umbali wa yadi 25.


    No 4: Arsenal v Bayer Leverkusen - Februari 27, 2002
    Bao lake la nne kwenye ushindi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya miamba ya Ujerumani, baada ya timu kutengeneza mashambulizi kutokea kwa Sylvain Wiltord ambaye alimpasia Bergkamp akiwa kwenye mstari wa goli, alichukua mpira huo kama anaenda pembeni na kumuangalia kipa akiwa ametoka nje kidogo ya lango kabla ya kuubetua mpira na kumpita Hans-Jorg Butt.


    No 3: Arsenal v Bolton - Mei 5, 1996

    Wakiwa wanahitaji kushinda ilikupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal walionekana kukaribia kupata sare, kabla ya Bergkamp kuchukua majukumu hayo begani kwake pale alipopokea pasi nzuri ya David Platt akiwa mita 25 nje ya goli, aligeuka kwa kasi ya ajabu na kuupiga mpira kwenda kwenye kona ya goli na kumshinda Keith Branagan na kuipa timu yake ushindi.


    No 2: Newcastle v Arsenal - Februari 3, 2002

    Ni bao ambalo alifanya kitendo ambacho, watu mpaka leo wanajiuliza alimaanisha kufanya ivo au aliotea tu. Lakini huyu ni Dennis Bergkamp. Ni lazima alimaanisha alichokifanya. Alijitengenezea nafasi nje ya eneo la hatari na kuomba mpira ambao alipasiwa na Robert Pires. Pasi ile ilipigwa nyuma yake lakini kwa kasi kubwa aliugusa mpira ule na mguu wake wa kushoto na kuzunguka akimpita Nikos Dabizas, na kumzidi nguvu beki mwingine kabla ya kukutana na mpira kwa mbele na kumfunga Shay Given kwa kutumia mguu wa kulia.


    No 1: Leicester v Arsenal - Agostio 27, 1997

    Hii ni moja kati ya hat-trick bora kwenye historia. Wakiwa na faida ya mabao mawili tayari, Bergkamp alifunga bao la tatu  kwenye dakika ya 90, akimalizia kazi ya David Platt akiwa ndani ya eneo la hatari aliumiliki mpira na mguu wake wa kulia kabla ya kutumia mguu wa kushoto kuvuta ndani mpira kumkwepa Matt Elliott. Hakushughulika na beki huyo hata pale alipovutwa shati kabla ya kuipiga shuti lililomshinda Kasey Keller. Mholanzi huyo analitaja hili kama bao lake bora zaidi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL KUWEKA SANAMU LA DENNIS BERGKAMP NJE YA UWANJA, ATAKUWA GWIJI MWINGINE WA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top