• HABARI MPYA

  Friday, February 22, 2013

  FERGUSON TAYARI KUMUONGEZEA MKATABA NANI KAMA MCHEZAJI WA BENCHI


  KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amempa masharti Nani kama anataka mkuendelea kubaki kwenye klabu hiyo, Mreno huo ameambia kama anataka kubaki inabidi akubali masharti ya mkataba mpya na pia akubali kukaa benchi.
  Nani, ambaye alisajiliwa na Man United kwa ada ya pauni milioni 17, kutoka Sporting Lisbon, mwaka 2007, mwakani anaweza kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru, ikiwa klabu haitafikia dau la mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki analolitaka.
  Hatahivyo, kiwango alichokionysha kwenye pambano la Kombe la FA dhidi ya Reading, akifunga bao moja na kutoa pasi ya bao la pili, kilimkumbusha Ferguson nini kinaweza kufanywa na Mreno huyo mwenye miaka 26.
  Talented: But Nani is far from one of the first names on Sir Alex Ferguson's team sheet
  Kipaji: lakini Nani hayupo kwenye majina ya kwanza ya Sir Alex Ferguson anapopanga kikosi
  “Ni wazi tunataka kumbakiza, ni mmoja kati ya wachezaji wenye akili ya ushindi zaidi ndani ya Ulaya nzima. Alisema Ferguson.
  “Anataka kuhakikishiwa namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini je anaweza kuhakikisha kiwango chake hakishuki, kiwango chake cha siku ile kinaweza kumhakikishia hilo. Tunajaribu kadri tuwezavyo kwa sababu ni mchezaji wa ushindi ambaye anaweza kufunga mabao mazuri.”
  Kama pande hizo mbili hazitafikia makubaliano, basi Unitesd watalazimika kumuuza nane, ambaye miezi michache iliyopita alikuwa na thamani ya pauni  milioni 25, sasa hivi wanaweza kumpoteza bure asipoangalia.

  Incoming: When Wilfried Zaha arrives in the summer, there will be even more pressure on Nani
  Wilfried Zaha ametua kumtia kashikashi Nani
  “Ni wazi tunataka kumbakiza, ni mmoja kati ya wachezaji wenye akili ya ushindi zaidi ndani ya Ulaya nzima. Alisema Ferguson.
  “Anataka kuhakikishiwa namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini je anaweza kuhakikisha kiwango chake hakishuki, kiwango chake cha siku ile kinaweza kumhakikishia hilo. Tunajaribu kadri tuwezavyo kwa sababu ni mchezaji wa ushindi ambaye anaweza kufunga mabao mazuri.”
  Kama pande hizo mbili hazitafikia makubaliano, basi Unitesd watalazimika kumuuza nane, ambaye miezi michache iliyopita alikuwa na thamani ya pauni  milioni 25, sasa hivi wanaweza kumpoteza bure asipoangalia. Walikuwa tayari kumuachia ajiunge na Zenit St Petersburg, Septemba, lakini alikataa baada ya mazungumzo na klabu hiyo. Pia alihusishwa na klabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Juventus, Porto na Arsenal. Toka kipindi hiko msimu huu umekuwa mgumu kwa ndani na nje ya uwanja Nani. 
  Ferguson alimtoa wakati wa mapumziki baada ya kuonyesha kiwango kibovu dhidi ya Liverpool  Septemba mwaka jana, na alimlaumu wazi wazi baada ya Man United kutolewa kwenye michuano ya Capital One Cup na Chelsea. 
  Nani alijikuta kwenye wakati mgumu zaidi na babu Fergie baada ya kumpiga ngumi kinda wa klabu hiyo Davide Petrucci, baada ya tukioa hilo akapata majeruhi ya kuchanika nyama za paja akakaa nje kwa miezi mitatu.

  Antonio Valencia
  Ashley Young
  Mawinga wengine: Antonio Valencia (kushoto) na Ashley Young (kulia) 
  Usajili wa pauni milioni 15 wa Wilfried Zaha kutoka Crystal Palace kumeongeza utata juu ya maisha ya baadaye ya Nani kwenye kalbu hiyo, huku Antonio Valencia na Ashley Young tayari wameshajihakikishia nafasi kama mawinga wa kikosi cha kwanza cha Man United.
  “Mbadala wake wako vizuri,” alisema Ferguson. “Valencia ameonyesha kiwango kikubwa sana kwetu, tuna Ashley Young ambaye anaweza kuchza kushoto pamoja na Ryan Giggs ambaye anaweza kuchza kushoto kwa staili ya aina yake. Inatufanya kuwa kwenye nafasi nzuri.
  Kocha wa United amethibitisha kwamba Wayne Rooney anaweza kukosa mechi ya Jumamosi dhidi ya QPR kutokana na kuwa majeruhi. Mshambuliaji huyo wa anaendelea kutumia dawa tunga alipoumia Jumamosi.
  Unwell: And Wayne Rooney could struggle to face QPR on Saturday
  Mgonjwa: Wayne Rooney anaweza kukosekana dhidi ya QPR kesho
  Ushindi Loftus Road utaifanya United kuongoza kwa tofauti ya pointi 15, kabla ya Manchester City kupambana na Chelsea, Jumapili na Ferguson  ameonywa kwamba wapinzani wake wa kesho wanatakiwa kushinda pambano lao ili kuweka hai matumaini yao uya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.
  Alisema: “Naweza kuelewa maono ya Man City kila siku wamesisistiza kwamba wanasubiri tupoteze pointi, lakini kiukweli kwamba na wao watapoteza pointi pia.”
  Wakati huo huo, Phil Jones anawakati mgumu kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya marudiano ya ligi ya mabinwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, huku Ferguson akiwa na matumaini madogo kwa kinda huyo kupona kwa wakati baada ya kuumia enka kwenye pambanao dhid ya Reading.
  Hana mpango wa kubadilisha staili ya kulinda ya Jones japokuwa mchezaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi toka alipotua United.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: FERGUSON TAYARI KUMUONGEZEA MKATABA NANI KAMA MCHEZAJI WA BENCHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top