• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 27, 2013

  WATOTO WA ABEDI PELE WABWAGA MANYANGA TIMU YA TAIFA GHANA  Jordan Ayew akishangilia na Andre Ayew.

  WATOTO wa Abedi Pele, Jordan na Andre, wametangaza wametangaza uamuzi wao wa kujiuzulu kwa muda kuchezea timu ya taifa ya  Ghana. Wawili hao wametuma taarifa kwa Chama cha Soka Ghana FA jana.

  Wote walikuwa wanadaiwa kuwa na mgogoro na viongozi wa FA.

  Andre Ayew
  Andre Ayew ameelezea matatizo yake binafsi na uongozi ya timu ya Black Stars yamemfanya ajiuzulu kwa muda. Amesema amevunjika moyo na nguvu kutokana na matatizo yake na uongozi na kwamba hawezi kuitumikia Ghana vizuri kwa sasa.
  "Uamuzi wangu wa kusitisha huduma zangu timu ya taifa  unatokana na matatizo kadhaa yaliyojitokeza hivi karibuni, hususan juu ya uhusiano wangu na uongozi wa timu ya wakubwa ya taifa, Black Stars."

  Jordan Ayew
  Wakati huo huo, Ayew mdogo anafikiri hakubaliki. Amesema licha ya kufanya vizuri, inaonekana uongozi haumjali.
  FA ya Ghana bado haijajibu barua za vijana hao, watoto wa gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WATOTO WA ABEDI PELE WABWAGA MANYANGA TIMU YA TAIFA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top