• HABARI MPYA

    Friday, February 22, 2013

    FIFA KUSIKILIZA MADAI YA ASAMOAH DHIDI YA YANGA

    Asamoah
    Na Boniface Wambura
    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limesema linapeleka rasmi madai ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Kenneth Asamoah kwenye chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) baada ya klabu hiyo kutojibu chochote.
    Awali FIFA ilipokea malalamiko ya Asamoah kuwa anaidai Yanga dola 5,000 za Marekani ambapo ilikuwa ni sehemu ya malipo yake (signing fee) baada ya kujiunga na klabu hiyo.
    Desemba mwaka jana FIFA iliiandikia barua Yanga kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka maelezo yake kuhusu madai hayo ya Asamoah, lakini hadi sasa haijajibu madai hayo.
    Kwa mujibu wa FIFA, hatua ya uchunguzi wa suala hilo umekamilika, na sasa linapelekwa rasmi katika chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) kwa ajili ya kufanya uamuzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FIFA KUSIKILIZA MADAI YA ASAMOAH DHIDI YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top