• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 19, 2013

  YANGA WAENDA BAGAMOYO MCHANA HUU KUJIANDAA NA MECHI NA AZAM JUMAMOSI

  Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts (kushoto) akiwafua wachezaji wake. Leo wanaenda Bagamoyo kujipanga kwa ajili ya Azam

  Na Mahmoud Zubeiry
  KATIKA kile kinachoonekana ni kuupa uzito zaidi mchezo dhidi ya Azam FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kikosi kizima cha Yanga kinaondoka mchana wa leo kwenda kuweka kambi Bagamoyo mkoani Pwani katika hoteli ya Kiromo.
  Msemaji wa Yanga SC, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba, kikosi hicho kinaondoka mchana wa leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, wanaoupa uzito mkubwa.
  Kizuguto amesema uongozi wa klabu hiyo na benchi la ufundi kwa ujumla pamoja na wachezaji, wanaipa uzito mkubwa mechi hiyo.
  “Mechi hii inapewa uzito mkubwa sana. Ni mechi ambayo lazima tushinde ili kuweka vizuri mazingira ya ubingwa, kwa sababu Azam ndio wapinzani wetu katika  mbio hizi,”alisema Kizuguto.
  Amesema hakuna majeruhi hata mmoja kwenye kikosi chao na wachezaji wana morali ya hali ya juu kuelekea mchezo huo.
  Kwa sasa, Yanga SC ndio inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 36, baada ya kucheza mechi 16, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 33.
  Hali ni mbaya kwa mabingwa watetezi, Simba SC wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi zao 28 hadi sasa, ingawa wamecheza mechi sawa na Yanga na Azam, 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA WAENDA BAGAMOYO MCHANA HUU KUJIANDAA NA MECHI NA AZAM JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top