• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 27, 2013

  BRANDTS LEO MECHI YA 20 YANGA DHIDI YA WABABE WAKE WA KWANZA ALIPOANZA KAZI TANZANIA


  Brandts
  Na Mahmoud Zubeiry
  KOCHA Mholanzi wa Yanga, Ernie Brandts leo anatarajiwa kuiongoza klabu hiyo katika mechi ya 20, tangu ajiunge nayo Septemba  mwaka jana akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet.
  Brandts, ambaye katika mechi 19 za awali, ameiwezesha Yanga kushinda  mechi 12, kufungwa nne na sare tatu, leo ataiongoza timu yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba.
  Mara tu alipojiunga na Yanga, mchezo wa kwanza kufungwa ulikuwa dhidi ya Wakata Miwa hao wa Misenyi, 1-0 na hadi sasa hiyo ndiyo timu pekee ya Tanzania, iliyowafunga Wana Jangwani chini ya Brandts.
  Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, kwa sasa anatembea kifua mbele, timu yake ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa pointi zake 39 ilizovuna kwenye mechi 17, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 36 na Simba SC 31.
  Brandts kwa sasa mafanikio yake yanachangiwa na sapoti kubwa ya uongozi wa timu yake, chini ya Mwenyekiti wake, Yussuf Manji.
  Baada ya kuifunga Azam 1-0 Jumamosi, ikitokea kwenye kambi ya Bagamoyo katika hoteli ya Kiromo, Yanga ilirejea kambini Jumatatu, lakini safari hii ikiwa ni hapa hapa mjini katika hoteli ya Tansoma.
  Kocha wa Kagera, Abdallah Kibadeni ameahidi kuifunga tena Yanga katika mchezo huo, ili nao wajivute juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, jambo ambalo linaashiria mchezo utakuwa mgumu.
  Katika mchezo huo, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, viingilio vinatarajiwa kuwa Sh. 5,000 (viti vya bluu na kijani), sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP C na B) na sh. 20,000 (VIP A).
  Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Toto Africans (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons (Manungu, Morogoro).

  REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA:
  Yanga 1-1 Simba SC         (Ligi Kuu) 
  Yanga 0-1 Kagera Sugar         (Ligi Kuu)
  Yanga 3-1 Toto African         (Ligi Kuu)
  Yanga 3-2 Ruvu Shooting         (Ligi Kuu)
  Yanga 3-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
  Yanga 1-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
  Yanga 3-0 JKT Mgambo (Ligi Kuu) 
  Yanga 2-0 Azam FC (Ligi Kuu)
  Yanga 2-0 Coastal (Ligi Kuu)
  Yanga 0-1 Tusker (Kirafiki) 
  Yanga 1-1 Ariminia Bielefed (Kirafiki)
  Yanga SC 0-2 Emmen FC (Kirafiki)
  Yanga SC 1-2 Denizlispor FC (Kirafiki)
  Yanga SC 3-2 Black Leopard (Kirafiki)
  Yanga SC 2-1 Black Leopard (Kirafiki) 
  Yanga SC 3-1 Prisons (Ligi Kuu)
  Yanga 1-1 Mtibwa Sugar         (Ligi Kuu)
  Yanga 4-0 African Lyon (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-0 Azam FC (Ligi Kuu)
  Yanga SC Vs Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BRANDTS LEO MECHI YA 20 YANGA DHIDI YA WABABE WAKE WA KWANZA ALIPOANZA KAZI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top