• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 28, 2013

  JKT RUVU YALICHIMBIA KABURI TOTO LA YANGA LIGI KUU

  Kikosi cha JKT Ruvu

  Na Prince Akbar
  JKT Ruvu ya Pwani, imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
  Ushindi huo, unaifanya JKT Ruvu itimize pointi 19, baada ya kucheza mechi 18, na kujiondoa kwenye maeneo ya hatari ya kushuka daraja.
  Kwa upande wa Toto, ambayo sasa inabaki na pointi zake 14 licha ya kucheza mechi ya 19 leo, kipigo hicho kinazidi kuwachimbia kaburi kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  Katika mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute, Wana Kishamapanda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 26, mfungaji Mwinja Magafu, ambalo lilidumu hadi mapumziko.
  Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, walisawazisha bao hilo dakika ya 52 kupitia kwa Ally Khan, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi kuifungia bao la ushindi timu yake dakika ya 71. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: JKT RUVU YALICHIMBIA KABURI TOTO LA YANGA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top