• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 23, 2013

  MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA YANGA NA AZAM TAIFA JIONI YA LEO

  Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall
  Na Mahmoud Zubeiry
  AZAM FC ilipanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2007/2008 na leo inacheza na Yanga SC kwa mara ya 10 tangu ipande katika ligi hiyo na kuleta changamoto kubwa katika soka ya Tanzania.
  Katika mechi tisa za awali, Azam imeshinda tatu, imefungwa nne na kutoa sare mbili.
  Katika mechi zote hizo, Azam imetikisa nyavu za Yanga mara 11, wakati zake zimetikiswa mara 13, huo ukiwa ni wastani wa kukusanya pointi 11, dhidi ya 14 za wapinzani wao hao.
  Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga ilishinda mabao 2-0, leo timu hizo zinarudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, je Azam italipa kisasi na kufanya pia idadi ya mechi za kufungana na wana Jangwani hao iwe sawa nne kwa nne?
  Bila shaka hilo na jambo la kusubiri na kuona, ila mchezo huo utakuwa mkali na wa kusisimua.

  MSIMAMO WA MATOKEO YA MECHI 
  ZA YANGA NA AZAM:
                    P W D L GF GA Pts
  Yanga SC 9 4 2 3 13 11 14
  Azam FC 9 3 2 4 11 13 11

  REKODI YA YANGA NA AZAM:
  Oktoba 15, 2007
  Yanga SC 3-1 Azam FC
  Aprili 8, 2008
  Azam FC 3-2 Yanga SC
  Oktoba 17, 2009
  Azam 1-1 Yanga SC
  Machi 7, 2010
  Yanga SC  2-1 Azam FC
  Oktoba 24, 2010
  Yanga SC 0-0 Azam FC
  Machi 30, 2011
  Yanga SC 2-1 Azam FC
  Septemba 18, 2011
  Azam 1-0 Yanga SC
  Machi 10, 2012
  Azam FC 3-1 Yanga SC
  Novemba 4, 2012
  Yanga SC 2-0 Azam FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MUHIMU KUJUA HAYA KABLA YA YANGA NA AZAM TAIFA JIONI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top