• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 28, 2013

  BOBAN NDANI MSAFARA WA SIMBA ANGOLA

  Simba na Libolo katika mechi ya kwanza Dar es Salaam, hapa wanaingia uwanjani

  Na Dina Ismail
  KIKOSI cha wachezaji 18 wa timu ya soka ya Simba kinatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho kwenda Luanda, Angola tayari kwa mechi yao ya marudiano ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Recreativo do Libolo ya huko utakaopigwa keshokutwa katika mji wa Caculo.
  Awali mchezo huo ilikuwa upigwe kesho mjini Luanda kabla ya kusogezwa hadi keshokutwa ambapo sasa utapigwa katika mji wa Caculo.
  Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba msafara wa timu hiyo utakaokuwa chini ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la  Soka Tanzania (TFF) Mohsin Balhabou utaondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).
  Aliwataja wachezaji walioondoka ni pamoja na Juma Kaseja, Abbel Dhaira, Nassor Said ‘Chollo’, Amir Maftah, Juma Nyosso, Shomari Kapombe, Komabil Keita, Salim Kinje, Kiggi Makassy, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi ‘Boban’, Mrisho Ngassa, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na Abdallah Juma.
  Aidha, Kamwaga aliwataja viongozi watakaoambatana na timu ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe, kocha Mkuu Mfaransa Patrick Liewig, kocha msaidizi Jamhuri kihwelo ‘Julio’ , Kocha wa makipa James Kisaka, Meneja Mosse Basena, Daktari Cossmas Kapinga na Mtunza vifaa, Kessy.
  Kamwaga alisema kocha mkuu wa timu hiyo, Liewing amekifanyia kazi kikosi chake kwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa awali, hivyo wana uhakika wa kuibukaa na ushindi ugenini.
  Simba ambayo ilifungwa bao 1-0 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo, inahitaji kushinda 2-0 ili isonge mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BOBAN NDANI MSAFARA WA SIMBA ANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top