• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 26, 2013

  GARETH BALE NI NOMA, AIPAISHA SPURS ENGLAND KWA BAO LA AJABU


  KOCHA Andre Villas-Boas amempigia debe Gareth Bale awe Mwanasoka Bora wa Mwaka, baada ya kuifungia Spurs bao la ushindi dakika ya mwisho, umbali wa yadi 25, dhidi ya West Ham na kuipeleka timu hiyo hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England. Spurs ilishinda 3-2.
  "Anacheza kwa kikubwa sana kwa sasa, ana kipaji babu kubwa, anastahili kushindania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka,amekuwa na msimu babu kubwa,"alisema kocha huyo wa Spurs. 
  Ecstasy: Tottenham's Gareth Bale celebrates scoring the fantastic winner
  Nyota wa Tottenham, Gareth Bale akishangiklia baada ya kufunga bao la ushindi
  Wonder shot: Bale's stunning strike shocked Upton Park as he stole the show to give a 3-2 win
  Bale akipiga shuti la bao la ushindi
  Bale aliifungia bao la kuongoza mapema Spurs kabla ya Andy Carroll na Joe Cole kuifungia The Hammers na kuifanya iongoze kwa 2-1. Lakini Gylfi Sigurdsson aliyetokea benchi akaisawazishia Spurs akifunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu kabla ya Bale kuipandisha Spurs juu ya Chelsea na kuzidi  Arsenal kwa pointi nne, wakielekea kukutana nayo Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: GARETH BALE NI NOMA, AIPAISHA SPURS ENGLAND KWA BAO LA AJABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top