• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 19, 2013

  TEKNOLOJIA KWENYE MSTARI WA LANGO KUTUMIKA KOMBE LA DUNIA MWAKANI


  SHIRIKISHO la soka Ulimwenguni (FIFA), limethibitisha matumizi ya Teknolojia ya Mstari wa Goli wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2014,  na wamekaribisha makampuni kuomba tenda ya kusambaza mfumo huo.
  Rais wa FIFA, Sepp Blatter, aliwahi kueleza dhamira yake ya kutaka teknolojia hiyo itumike wakati wa michuano hiyo nchini Brazil, hii ikiwa ni miaka 50 tangu bao la utata la Geoff Hurst lilipofungwa mwaka 1966 wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.
  Teknolojia hiyo ilijaribiwa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, Disemba mwaka jana, FIFA sasa hivi wanatarajia kuanza kuitumia katika michuano ya Kombe la Mabara, wakati wa majira ya joto, na wakati wa Kombe la Dunia.

  Football, FIFA Club World Cup Japan, Goal line technology
  Football, FIFA Club World Cup Japan, Goal line technology
  Majaribio: Kipa wa Chelsea, Petr Cech akijaribu teknolojia ya mstari wa Goli, wakati Kombe la Dunia la Klabu.

  Taarifa ya FIFA ilisema: “Baada ya kufanikiwa kwa matumizi wa Teknolojia ya Mstari wa Goli (GLT) wakati wa Kombe la Dunia la Klabu, nchini Japan, Disemba 2012, FIFA imeamua kutumia GLT kwenye Kombe la Mabara nchini Brazil mwaka 2013 na Kombe la Dunia nchini Brazil 2014.
  “Dhumumi la kutumia GLT ni kuwasaidia waamuzi wa mechi na kufunga mfumo huu kwenye viwanja vyote, tunasubiri mafanikio kwenye ufungaji na mazoezi ya uamuzi kabla ya mechi.
  “Kukiwa na teknolojia mbalimbali sokoni, FIFA imetangaza tenda leo, tumeweka vitu tunavyovitaka kiufundi kwa ajili ya mashindano mawili ya FIFA yajayo nchini Brazil.”
  Controversial: Debate has raged for almost 50 years over Geoff Hurst's goal in the 1966 World Cup final
  Utata: Mjadala umekuwepo kwa karibu miaka 50, juu ya bao la Geoff Hurst wakati wa Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966.

  Teknolojia za Hawk-Eye na GoalRef zote zimeshapitishwa na FIFA na zinajipanga kupambana kati ya zenyewe kwa zenyewe na kama ikiwezekana dhidi ya teknolojia zingine kupata haki ya Kombe la Dunia.
  HawkEye inajumuisha matumizi ya kamera, wakati GoalRef ina mfumo wa kisayansi zaidi, ikijumuisha sehemu ndogo ya sumaku inayowekwa kulizunguka goli na vifaa vya umeme kwenye mpira, huku taarifa ya bao ikisafirishwa kwa sekunde chache mpaka kwenye saa inayovaliwa na mwamuzi.
  FIFA ilisema: “Watoaji wawili wa GLT tayari wameshapewa leseni chini ya Mpango wa Ubora wa FIFA kwa ajili ya GLT, na wasambazaji wengine wa GLT kwa sasa wako kwenye mchakato wa kupata leseni (wale waliovuka majaribio yote muhimu) wanakaribishwa kuleta tenda zao.

  Taarifa za mifumo miwili

  HAWK-EYE
  Huu ni Mfumo wa Kamera, umezalishwa na Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye, ambayo ilinunuliwa mwaka jana na Kampuni ya Japan ya Sony, ambao tayari wanamfumo unaotumiwa kwenye mchezo wa tenesi na Kriket.
  Kamera sita au saba za kurekodi matukio kwa kasi, zinafungwa pande zote za uwanja, kwenye Paa la kiwanja, zinafuatilia uwepo wa mpira na mfumo wa kompyuta unafanya mahesabu na kujua wapi mpira upo uwanjani, na kutuma maseji za umeme kwenye kifaa kama saa ambacho kinavaliwa na mwamuzi uwanjani, pale mpira unapovuka mstari.
  Swali pekee juu ya mfumo huu wa Hawk-Eye, ni je, utaweza kufanya kazi kwenye matukio machache sana ambayo mwili wote wa kipa utakuwa umefunika mpira.
  FIFA wamesisitiza kwamba picha hizo hazitaonyeshwa kwenye televisheni kubwa za uwanjani, baada ya tukio lolote la utata, huku mwamuzi pekee ndiyo akishituliwa kama mpira umevuka mstari ama la.

  GOALREF
  Mfumo huu umetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Wadenmark na Wajerumani, GoalRef inatumia eneo la sumaku kutambua kama mpira umevuka mstari ama la. Mistari mitatu ya sumaku inawekwa kwenye maungio ya mpira, kati kati ya bladder na nje, na pale mpira ukivuka mstari hizi zinatambuliwa na Vifaa maalumu vya ufahamu ambavyo vinakuwa kwenye miamba ya goli.
  Vifaa hivyo vvya fahamu, vinatuma mawimbi ya umeme ambayo yanavurugwa pale mpira utakapo vuka mstari wa goli na kompyuta inatuma ujumbe kwa mwamuzi, kupitia kwenye saa ambayo amevaa ndani ya sekunde moja.
  Ufungaji wa mfumo huu siyo wa bei kali sana kama Hawk-Eye lakini bado ni muhimu. Hapa kinachobakia ni masuala ya kujadili na watengenezaji wa mpira kuruhusu uwekwaji wa mstari hiyo ya sumaku kwenye mpira, lakini tayari GoalRef wameshazungumza na watengeneza wa mipira.
  Shocker: Frank Lampard was denied a clear goal during England's quarter final with Germany in 2010
  Haamini: Frank Lampard alinyimwa bao la waza wakati wa robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani mwaka 2010.
  Shocker: Frank Lampard was denied a clear goal during England's last-16 clash with Germany in 2010
  Manuel Neuer of Germany watches the ball bounce over the line
  “Kampuni za GLT ambazo zitakuwa tayari zitaalikwa wakati wa ukaguzi wa viwanja vya Kombe la Mabara, tukio hilo kwa sasa limepangwa kufanyika kati kati ya Machi, huku uamuzi wa mwisho ukitarajiwa kutolewa mwanzoni mwa Aprili.”
  Uamuzi wa FIFA umekuwa kama kioo kwa Ligi Kuu ya England wanaopanga kuitumia teknolojia hiyo kwenye msimu ujao.
  Baada ya utata kibao – ikiwa pamoja na bao la Frank Lampard dhidi ya Ujermani wakati wa Kombe la Dunia la 2010- soka sasa liko tayari kubadilika, Bodi ya Vyama vya Soka (IFAB), imeshatoa baraka zao kwa teknolojia za Hawk-Eye na GoalRef wakati wa mkutano wao uliofanyika Zurich mwaka jana.

  Sepp Blatter
  Sepp Blatter
  Uamuzi: Rais wa FIFA, Sepp Blatter amekubalia matumizi ya teknolojia


  Ligi Kuu ya England iliapa kuleta teknolojia hiyo muda mfupi baada ya uamuzi wa IFAB.
  Kombe la Dunia la Klabu, lililofanyika Tokyo, ambalo Chelsea walishiriki ilikuwa michuano ya kwanza kutumia teknolojia hiyo.

  Jinsi michezo mingine ilivyoonyesha njia

  KRIKETI
  Mchezo huu ndio ulikuwa wa kwanza kuanza kutumia maamuzi ya teknolojia, walianza kufanya hivyo miaka 20 iliyopita, teknolojia kama Hawk-Eye zinatumiaka ambapo wachezaji wanaweza kupingana na uamuzi wa refa na kuomba kuangalia marudio ya televisheni.

  TENISI
  Wanaofuatilia michuano ya Wimbledon watakumbuka matumizi ya Cyclops, mfumo wa infrared, ulitumika kuangalia kama mpira umevuka mstari ama la, ulitambulishwa mwaka 1980. Siku hizi wanatumua Hawk-Eye, mfumo ambao unaangalia mpira ulipo uwanjani na kutoa maamuzi, wanaita maamuzi hayo marudio ya Hawk-Eye, yanasaidia kutoa maamuzi sahihi

  LIGI YA RAGBI
  Uamuzi wa video ulikuja kwenye Ligi ya Rugby, mwaka 1996 na imekuwa sehemu ya mashindano, japokuwa imekuwa ikibadilika kadri miaka inavyokwenda mbele, lakini uamuzi wa video unatoa maamuzi mengi.

  MUUNGANO WA RAGBI 
  Huku wanatumia Mwamuzi wa Televisheni, hii ilianza mwaka 2001. Hutumiwa kwenye mashindano makubwa tu, japokuwa inashindwa kutoa maamuzi kwenye mambo mengi inaamua kwenye masuala ya goli tu.

  MPIRA WA MIGUU WA KIMAREKANI
  NFL ilitambulisha mfumo wa marudio mwaka 1986, kukiwa na mwamuzi wa ziada akitumika kuangalia marudio ya picha za televisheni na kutoa maamuzi. Mfumo huu uliachwa mwaka 1992, ukabadilishwa na ikawa mwamuzi mwenyewe wa kati ndiye anayeenda kuangalia marudio ya picha za televisheni, anatakiwa kufanya maamuzi ndani ya sekunde 60 baada ya kuangalia picha za marudio.

  Historia fupi ya mabadiliko kwenye soka

  1863: wakati wa mkutano ukumbi wa Freemasons uitwao Tavern, London, FA walianzisha sheria kadhaa. The Cambridge Rules – hii ilitengenezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge katika miaka ya 1890, zinaandikwa upya na kuja kwa mara ya kwanza na sheria ya kuvaa jezi.
  1869: Goal-kicks inaanzishwa na kona zinafuata miaka mitatu baadaye.
  1875:  Mwamba wa juu unabadilisha matumizi ya kamba kwenye eneo la juu la goli.
  1878: Mwamuzi anatumia filimbi kwa mara ya kwanza.
  1882: Vyama vya Soka vya Uingereza vinaunganisha sheria zao na kuanzisha IFAB – bodi ya kuangalia Sheria za Soka.
  1891: Penalti zinapigwa kwa mara ya kwanza, uwekwaji wa wavu golini unakubalika kwenye sheria za soka na mwamuzi anaruhusia kusimama katikati ya uwanja.
  1902: Boksi la penalti linatambulishwa hii ilikuwa baada ya uwamuzi wa kutoa penalti pale faulo inapofanyika ndani ya mita 18 kutoka kwenye mstari wa goli na mita 44 kwa upana. Boksi la mita sita pia linatambulishwa, japokuwa inatumia miaka mingine 35 kwa D kuchorwa nje ya 18.
  1912: Makipa wanazuiwa kudaka mpira nje ya boksi la penalti.
  1925: Sheria ya Kuotea – wachezaji wanahesabika kwamba hawajaotea kama kuna wachezaji watatu kati ya mpira na goli – baadaye wanapunguzwa na kubaki wawili.
  1938: Sheria za soka zinatengenezwa na  mwanachama wa IFAB, Stanley Rous, ambaye alifanya kazi kubwa sasa, sheria hizo zilipitiwa upya tena mwaka 1997.
  1958: Wachezaji wa akiba wanaruhusiwa kwa mara ya kwanza, hii ikiwa ni kwa kipa aliyeumia na wachezaji walioumia tu.
  1970: Kadi nyekundu na njano zinatambulishwa kwenye soka wakati Kombe la Dunia la mwaka 1970 nchini Mexico.
  1990: Sheria ya kuotea inabadilishwa, sasa hivi anahesabiki hajaotea kma yuko sawa na beki wa mwisho.
  1992: Makipa wanakatazwa kudaka mpira uliorudishwa na wachezaji wa timu zao kwa kutumia mguu.
  1994: Eneo la Benchi la ufundi linatambulishwa kama ni sehemu ya sheria za soka, mwamuzi wa akiba anaongezwa mwaka unaofuata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TEKNOLOJIA KWENYE MSTARI WA LANGO KUTUMIKA KOMBE LA DUNIA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top