• HABARI MPYA

  Tuesday, February 19, 2013

  MSHAMBULIAJI EL MERREIKH AKABIDHIWA JEZI YA SIMBA

  Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Simba SC, Abdulfatah Salim Saleh akimkabidhi zawadi ya jezi ya Simba SC, mshambulaji wa Al Nasir ya Sudan, Kun James baada ya kukoshwa na soka yake Jumamosi, timu hiyo ilipocheza na Azam FC na kulala 3-1 katika Kombe la Shirikisho Afrika. James ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Sudan Kusini, ndiye aliyekuwa akiisumbua mno ngome ya Azam siku hiyo na ndiye aliyetoa pasi ya bao la Nasir, lililofungwa na Fabian Elias.
  James ametua Nasir msimu huu akitokea El Merreikh ya Sudan, aliyoichezea kuanzia mwaka 2010, alipojiunga nayo akitokea El Gouz iliyomuibua mwaka 2007.
  James mwenye umri wa miaka 25, anasema anapenda kucheza nje ya kwao na yuko tayari kusaini timu yoyote ya hapa Tanzania itakayomuhitaji.

  Abdulfatah akiwa ameketi na James ofisni kwake, Sapphire Court Hotel

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI EL MERREIKH AKABIDHIWA JEZI YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top