• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 26, 2013

  EPIQ STARS KUWASHA MOTO MAISHA CLUB DAR IJUMAA HII

  Nyota wa EBSS

  Na Prince Akbar
  ZIARA ya kuzindua nyimbo za wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq BSS itaendelea tarehe 1 mwezi wa tatu, ijumaa hii katika ukumbi wa Maisha Club Dar ambapo wasanii wote walioingia kumi bora wanatarajiwa kufanya show kali siku hiyo.
  Wasanii hao ambao wiki iliyopita walifanya show kali katika ukumbi wa Maisha Club Dodoma, wanatarajiwa pia kufunika Maisha Club. Wasanii hao ambao wengi wamekuwa wakisubiriwa kwa hamu na wengi tokea shindano lilipoisha mwishoni mwa mwaka jana wamekuwa wakizungumziwa na wengi kama wanamziki watakaofanya vizuri mwaka huu.
  Wasanii watakaofanya show Dar ni Menina Atick, Nsami Nkwabi, Nshoma, Vincent, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
  Huku baadhi ya nyimbo zikiwa tayari zinafanya  vizuri kwenye soko la muziki kama wimbo mpya wa Walter-Siachi, Menina-Dream Tonight, Husna-Nawamimina, Wababa-My Wife na Nsami- Muongo usiku huo pia utakuwa na vitu vipya kibao, pamoja na uzinduzi wa nyimbo mpya za Norman, Nshoma, Vincent na Godfery.
  Akizungumzia show hiyo,mmoja wapo wa wasanii hao, Walter anasema wapenda burudani wa Dar wasikose kuja kumshuhudia yeye na wasanii wengine wa Epiq BSS wakifanya vitu vyao kwani wamejipanga kwa muda mrefu.
  ‘Pamoja na wimbo wangu wa Siachi pia mashabiki watapata fursa ya kuusikia wimbo wangu utakaoufuata siku hiyo hiyo’ alisema Walter, ambaye alifanya show kali sana Dodoma.
  Usiku huo pia utapambwa na burudani kali kutoka kwa wakali wengine kama Ben Paul, Barnaba, Linah na Rich Mavoko.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: EPIQ STARS KUWASHA MOTO MAISHA CLUB DAR IJUMAA HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top