• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 22, 2013

  ISIHAKA HASSAN 'CHUKWU' ASEMA YONDAN NI BEKI BORA TANZANIA KWA SASA

  Isihaka Hassan 'Chukwu'

  Na Mahmoud Zubeiry
  BEKI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Isihaka Hassan ‘Chukwu’ amesema kwamba anavutiwa na uchezaji wa beki wa kati wa Yanga, Kevin Yondan na kwamba huyo ndiye beki bora kwa sasa nchini.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY wiki hii, Chukwu alisema kwamba kuna tatizo la mabeki wa kati kwa sasa nchini, lakini Yondan ni beki bora.
  “Ni haki yake kugombewa na Simba na Yanga, huyu kijana ni mchezaji mzuri, anacheza vizuri na kama ataendelea kuwa chini ya walimu bora na wepesi, atazidi kuwa bora,”alisema Chukwu.
  Hata hivyo, Chukwu amemuasa Yondan ambaye wenzake wanamuita Cotton Juice kwa jina la utani, kuepukana na vitendo ambavyo vitaangusha soka yake.
  “Yondan lazima ailinde soka yake kwa kuepuka anasa na utumiaji wa dawa za kulevya, hayo ni mambo ambayo akiyafanya yatammaliza mara moja, mimi namkubali sana,”alisema Chukwu.
  Chukwu ni mmoja kati ya mabeki hodari wa kati kuwahi kutokea nchini, ambaye alirithi mikoba ya Leodegar Chillah Tenga katika timu ya taifa.
  Alisajiliwa Yanga moja kwa moja kutoka ‘mchangani’, kutokana na sifa zake kuenea kwamba anacheza kama Chukwu wa  Nigeria.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ISIHAKA HASSAN 'CHUKWU' ASEMA YONDAN NI BEKI BORA TANZANIA KWA SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top