• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 20, 2013

  HII NI SILAHA YA SIRI YA AC MILAN DHIDI YA BARCA LEO?  Silaha ya siri ya AC Milan?

  Italian glamour model Claudia Romani playing football in an AC Milan jersey and black thong bikini
  Mwanamitindo wa Italia, Claudia Romani anaonekana yuko tayari kwa pambano dhidi ya Barcelona...

  KOCHA WA AC Milan, Massimiliano Allegri alisema anakaribisha mawazo ya uteuzi wa timu na mbinu kutoka kwa Rais wa klabu hiyo Silvio Berlusconi, akiongeza kusema kwamba timu yake haitakubali kuwa Mbuzi wa Kafara kwenye Ligi ya Mabingwa wakati wa pambano lao dhidi ya Barcelona.
  Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Berlusconi mra kwa mara amekuwa akiongelea juu ya masuala ya upangaji wa timu, jambo limekuwa likitokea kwenye timu nyingi.
  Wazo lake la hivi karibuni lilikuwa kwamba AC Milan imkabe Lionel Messi kwa staili ya mtu na mtu kwenye pambano la leo usiku, katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja wa San Siro.
  Advice: Milan head coach Massimiliano Allegri welcomed the help of president Silvio Berlusconi
  Ushauri: Kocha wa AC Milan, Massimiliano Allegri amekaribisha msaada kutoka kwa Rais Silvio Berlusconi
  Midfielder: Riccardo Montolivo addresses the media ahead of the Barcelona tie
  Kiungo: Riccardo Montolivo akiongea na vyombo vya habari kabla ya pambano dhidi ya Barcelona

  “Nimekaa chini na kuzungumza na Rais juu ya mechi hii” alisema Allegri. “Kama kawaida yake alitoa mawazo yake, ambayo kuna wakati ni mazuri na yamepokelewa.
  “Nitajaribu kutumia mfumo bora zaidi, ilitupate matokeo mazuri, na hilo ndilo linatakiwa.”
  AC Milan, ambao waliuza wachezaji wao wenye majina makubwa mwisho wa msimu uliopita na kupunguza gharama, ni mabingwa mara saba wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini sasa hivi wanajenga timu mpya na wanaonekana kama vibonde kwenye hatua ya 16 bora.

  Getting ready: Allegri talks to his players during a training session on Tuesday

  Muwe tayari: Allegri akiongea na wachezaji wake wakati wa mazoezi jana. 
  Mario Balotelli
  Mario Balotelli
  Hachezi: Mario Balotelli alianza kwa kasi maisha yake AC Milan, lakini atakosekana kwenye mechi ya leo.
  Threat: Forward Stephan El Shaarawy trains at the Milanello training centre
  Tishio: Mshambuliaji Stephan El Shaarawy akiwa mazoezini 
  Danger: Italian striker Giampaolo Pazzini in action during training
  Hatari: Mshambuliaji wa Italia Giampaolo Pazzini akiwa mazoezini

  “AC Milan dhidi ya Barcelona inamaanisha tunakutana na timu bora duniani, lakini sikubaliani na watu kutuona sisi kama Mbuzi wa Kafara” alisema Allegri. 
  AC Milan ilikutana na Barcelona kwenye hatua ya makundi na Robo fainali ya michuano hiyo msimu uliopita lakini walishindwa kushinda mechi hata moja kati ya mechi nne walizocheza wakitoka sare mbili na kufungwa mbili.
  “Kwenye miaka miwili iliyopita tumecheza vizuri dhidi ya Barcelona,” alisema Allegri, ambaye huu ni msimu wake wa tatu akiwa kiongozi wa miamba hiyo ya San Siro huku akishinda taji la Serie A mara moja.

  Optimistic: Allegri said Milan have played well against Barcelona over the last two seasons
  Anajiamini: Allegri amesema walicheza vizuri dhidi ya Barcelona katika mechi zilizopita 
  Preparation: Barcelona trained at the San Siro on Tuesday night
  Maandalizi: Barcelona wakifanya mazoezi San Siro, Jana usiku
  Star: Lionel Messi will be on show at the San Siro on Wednesday
   Staa: Lionel Messi atakuwa uwanjani San Siro, leo

  “Tunajua kwa sasa ndiyo timu bora duniani, lakini tunatakiwa kujaribu na kutengeneza mazingira ya kusonga mbele hadi hatua inayofuata, japokuwa, tunajua kwamba timu yoyote wanayocheza nayo huwa wanamiliki mpira kwa asilimia 65.
  “Tunatakiwa kujaribu kuzuia umiliki wao wa mpira, na kuwafanya wasiwe hatari sana kwa sababu huwa wanatisha zaidi wakati wakishambulia.” Alisema
  Mechi hiyo itakuwa ya kipekee kwa mshambuliaji wa AC Milan, Bojan Krkic, ambaye amekuliwa kwenye klabu ya Barcelona, akiwafungia mabao 41 katika mechi 163.

  Leader: Barcelona captain Carles Puyol attends a press conference on the eve of the tie
  Kiongozi: Nahodha wa Barcelona Carles Puyol akizungumzia mchezo huo
  Team: Barcelona coach Jordi Roura talks to his players during training at the San Siro
  Timu: Kocha wa Barcelona, Jordi Roura akijadiliana na wachezaji wake San Siro, jana


  Mario Balotelli, ambaye amefunga mabao manne katika mechi tatu, tangu alipotua kwenye klabu hiyo akitokea Manchester City, mwezi uliopita, hataruhusiwa kucheza pambano la leo, kwa sababu alishaiwakilisha Man City kwenye michuano hiyo.
  Kiungo wa Barca, Xavi Hernandez yuko tayari kwa pambano hilo baada ya kukosekana kwa wiki mbili, akisumbuliwa na majeruhi. Mshambuliaji wa David Villa, atakosa mchezo huo baada ya kutumia muda mwingi wa wiki iliyopita akisumbulia ugonjwa wa Figo kuuma.  Adriano atakosa pambano hilo kutokana na kuumia mguu wake wa kulia. Hata hivyo, Barcelona watakuwa na Lionel Messi. 
  Dancing moves: Xavi performs some peculiar stretches

  Zoezi: Xavi akinyoosha viungo vyake. 
  All smiles: Messi and Javier Mascherano have fun during training

  Tabasamu: Messi na Javier Mascherano wakitania wakati wa mazoezi
  World class: Spanish midfielder Andres Iniesta gets ready for the away leg on Wednesday

  Kiwango: Andres Iniesta akijipanga kwa ajili ya pambano la leo


  Utakuwa wakati uliojaa hisia kwa kocha wa muda wa Barca, Jordi Roura ambaye amerudi kwenye uwanja ambao alipata majeraha yaliyomlazimisha kuachana na soka.
  Anaiongoza Barca kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora, kutokana kukosekana kwa Tito Vilanova, ambaye anaendelea kujiuguza kutokana na kufanyiwa upasuaji wa koromero, Miaka 23 iliyopita Roura alipata majeraha ya goti lake wakati klabu hizo zilipokutana kipindi hicho.
  Japokuwa Roura, ambaye alikuwa na umri wa miaka 22 wakati huo, aliendelea kucheza soka kwa miaka kadhaa mbele, hakufanikiwa kurudia kiwango chake na alizunguka kwenye klabu ndogo za Murcia, Figueres na Sant Andreu kabla ya kutundika daluga.
  Superpower: Barcelona have won the Champions League three times since 2006

  Majembe: Barcelona wameshinda Ligi ya Mabingwa mara tatu tangu mwaka 2006
  Superpower: Barcelona have won the Champions League three times since 2006

  “Sina kumbukumbu nzuri kwenye mechi dhidi ya Milan, miaka 23 iliyopita,” alisema Roura
  “Baada ya kupata majeruhi sikuweza kucheza  soka tena. Milan walikuwa na bonge la timu wakati ule. Nimerudi hapa mara nyingi tangu kipindi kile nikiwa kwenye benchi la ufundi la Barca. Ni mengi yametokea tangu wakti huo, maisha kila siku yanakupa nafasi za ziada,” aliongeza Roura.
  “Siku zote ni nzuri sana kwa mtu anayependa soka kuja kwenye uwanja huu, siku zote inaogopesha kucheza na Milan hapa.”
  Roura amekuwa na maisha ya ukimya ya ukocha, kabla ya kupandishwa kwenye jukumu hilo kubwa shukurani ziuendee mfumo wa Barca wa kudumisha umoja ambao hupandisha watu kutoka ndani ya klabu. 
  Pale Pep Guardiola alivyochukua mikoba ya Barca, Roura alijiunga na timu hiyo akipewa jukumu la kuangalia wapinzani wajao wa timu hiyo lakini tangu wakati huo amepanda cheo.
  Je, hii ndio silaha ya siri ya Milan?
  Italian glamour model Claudia Romani playing football in an AC Milan jersey and black thong bikini
  Italian glamour model Claudia Romani playing football in an AC Milan jersey and black thong bikini

  Staa aliyefichwa? Mwanamitindo wa Italia, Claudia Romani alicheza soka akiwa na jezi ya Milan na bikini nyeusi jana 
  Model: Romani practiced her ball skills ahead of Wednesday's Champions League showdown

  Mwanamitindo: Romani alifanyia mazoezi uwezo wake wa kukaa na mpira, kuelekea kwenye pambano la leo.

  Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2281399/AC-Milan-v-Barcelona-Italians-bikini-clad-model-training-them.html#ixzz2LQtFItee
  Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: HII NI SILAHA YA SIRI YA AC MILAN DHIDI YA BARCA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top