• HABARI MPYA

    Monday, February 18, 2013

    SIMBA NA LIBOLO YAINGIZA MILIONI 133, AZAM NA NASIR MILIONI 34 PRIME TIME WACHUKUA MILIONI 29

    Haruna Moshi 'Boban' wa Simba, akimtoka beki wa Libolo jana

    Na Boniface Wambura
    PAMBANO la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Libolo FC ya Angola lililofanyika jana (Februari 17 mwaka huu) limeingiza sh. 133,795,000 wakati lile la Kombe la Shirikisho kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini lililochezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) limeingiza sh. 34,046,000.
    Watazamaji 22,469 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Simba kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Simba ilipoteza pambano hilo kwa bao 1-0.
    Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za waamuzi sh. 24,926,500, gharama za tiketi sh. 7,410,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za waamuzi na tiketi ilikuwa sh. 15,218,775, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 10,145,850 na asilimia 75 iliyokwenda klabu ya Simba ni sh. 76,093,875.
    Mechi ya Azam iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ilishuhudiwa na watazamaji 13,431 kwa viingilio vya sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000. Mgawo katika mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo;
    Gharama za tiketi sh. 4,779,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za tiketi ilikuwa sh. 4,390,050, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,926,700 na asilimia 75 iliyokwenda Prime Time Promotions (Azam) ni sh. 29,267,00.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA NA LIBOLO YAINGIZA MILIONI 133, AZAM NA NASIR MILIONI 34 PRIME TIME WACHUKUA MILIONI 29 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top