| Kocha Mkuu wa Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig (kushoto) saa 9:20 alikuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kupanga vifaa vya mazoezi kwa ajili ya mazoezi ya timu hiyo yanayoanza saa 10:00 jioni. Kulia ni Meneja wa Vifaa vya Michezo vya klabu hiyo, Kessy Rajab akimsaidia kocha huyo. Leiwg ni mtu mwenye juhudi na kazi yake na wakati wote amekuwa akifika wa kwanza mazoezini, japokuwa ana wasaidizi watatu, Jamhuri Kihwelo, James Kisaka na Mganda Moses Basena. |