• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 23, 2013

  YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI

  Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiwa amedaka mpira mbele ya kiungo wa Azam FC, Humphrey Mieno na nyuma yake ni kiungo mwingine wa timu hiyo, Khamis Mcha 'Vialli', huku beki wake, Kevin Yondan (kushoto) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0.

  Wachezaji wa Yanga, kutoka kulia Haruna Niyonzima, Oscar Joshua na Athumani Iddi 'Chuji' wakijadiliana wakati mchezo uliposimama kwa muda ili Barthez atibiwe baada ya kuumia

  Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Kevin Yondan.

  Niyonzima (8) aliyeshikana mikono na Hamisi Kiiza akielekea eneo la mashabiki wa Yanga kushangilia baada ya kufunga

  Mabeki; David Mwantika wa Azam mbele akikabiliana na Kevin Yondan wa Yanga

  John Bocco akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' 

  Mchezaji bora wa mechi ya leo; Haruna Niyonzima akiwa ameupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah 

  Hamisi Kiiza kushoto akigombea mpira na David Mwantika, kulia ni Chuji na Salum Abubakar 'Sure Boy'

  Jerry Tegete akipiga shuti huku David Mwantika akiweka mguu

  Kipa Ally Mustafa 'Barthez' akiinuka baada ya kutibiwa na Daktari, Nassor Matuzya. Mbele yake ni Yondan akimfuatilia

  Simon Msuva akienda chini baada ya kupigwa kwanja na beki wa Azam

  Kikosi cha Azam leo 

  Kikosi cha Yanga leo

  Barthez amelala chini baada ya kuumia, huku mshambuliaji wa Azam, John Bocco 'Adebayor' akizungumza na refa Hashim Abdallah


  Niyonzima akimtoka Mieno

  Barthez anadondoka na mpira baada ya kuudakia juu

  Hamisi Kiiza akimueleza jambo beki wa Azam, Mwantika wakati kipa Mwadini Ally akiwa amelala chini baada ya kuumia. Wengine kushoto ni Didier Kvumbangu na refa Hashim Abdallah

  Barthez akiwapanga mabeki wake (hawapo pichani) wakati Azam wanapga mpira wa adhabu

  Kavumbangu akipasua ukuta wa Azam

  Kiiza kushoto akiwatoka mabeki wa Azam

  Chuji akinawa maji kupoza mishipa ya kichwa

  Kocha wa Azam, Stewart Hall akitoka uwanjani kinyonge baada ya mechi

  Refa Hashim Abdallah akisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi 

  Wachezaji wa Azam wakimzonga refa wakimtuhumu kumaliza mechi kabla ya muda

  Kocha wa Yanga, Ernie Brandts wa Uholanzi akiwapungia mikono mashabiki wake baada ya mechi

  Hamisi Kiiza kulia akigombea mpira na beki Joackins Atudo wa Azam

  Msuva akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam

  Joackins Atudo akimuondoa njianui Msuva 

  Jerry Tegete akimtoka Salum Waziri wa Azam

  Tegete amepiga tik tak mbele ya mabeki wa Azam

  Niyonzima akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Azam

  Niyonzima anamtoka Mcha

  Niyonzima anamtoka Mcha

  Viungo bora; Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam akigombea mpira na Frank Domayo wa Yanga. Nyuma ni Chuji akiwa tayari kuingilia

  Sure Boy anaambaa na mpira pembeni ya Tegete

  Frank Domayo akimvisha kanzu Kipre Tchetche

  Sure Boy anamtoka Kavumbangu

  Sure Boy anawatoka viungo wa Yanga Domayo na Chuji kulia. Mbele ni Yondan

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top