• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 21, 2013

  CHELSEA YAIFUMUA BARCELONA 2-0 KOMBE LA VIJANA ULAYA


  MABAO ya Islam Feruz na Jeremie Boga yaliisaidia Chelsea ya vijana chini ya umri wa miaka 19 kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Barcelona ya umri huo na kusonga mbele hadi hatua ya robo fainali ya michuano ya Next Gen series.
  Licha ya Connor Hunte kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya pili tu ya kipindi cha pili, the Blues walikomaa kabla ya Boga kufunga bao la juhudi binafsi katika dakika za majeruhi.
  Bao hilo liliwachanganya zaidi Barcelona, huku Frank Bagnack akimbabua mpira wa kichwa George Saville wakati wa akisherekea.

  Opener: Islam Feruz got proceedings underway for Chelsea
  Bao la kwanza: Islam Feruz alifungua shughuli kwa Chelsea

  Mechi ilitawaliwa na ubabe wa hapa na pale lakini hilo halikuzuii kuona kiwango bora kilichonyeshwa na vijana.
  Feruz alifunga bao la kwanza, akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na wachezaji wenzake.
  Todd Kane, ambaye alikuwa na mchezo mzuri na ndiye aliyemtengenezea Feruz bao, aliokoa mpira kwenye mstari wa lango lao wakati Barca walipojaribu kujitengenezea kupata bao la mapema.
  Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Mini Estadi ilianza saa 11 jioni muda wa England, ilikupisha mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya AC Milan na Barcelona ya wakubwa, ilishuhudia Wahispaniola hao wakilisakama lango la The Blues wakitafuta bao la kusawazisha.
  Hunte alitolewa nje baada ya kupata kadi ya pili ya njano, kutokana na mchezo mbaya, kadi nyekundu ya kinda hiyo inamfanya afuate nyayo za Magwiji wa Chelsea John Terry na Didier Drogba, ambao nao waliwahi kupata kadi nyekundu dhidi ya Barcelona.
  Barca walianza kusaka bao kwa nguvu, huku David Babunski akipiga tik tak ambayo ilipita pembeni kidogo ya lango la Adam.
  Lakini wakati Narca wakishambulia walijisahau na Chelsea wakapata bao la pili, zikiwa zimesali dakika mbili tu pambano hilo kuisha, baada ya Boga kujitengenezea nafasi na kupiga shuti kali lililoenda moja kwa moja wavuni.
  Ijumaa ndiyo ratiba ya hatua ya robo fainali itapangwa na Chelsea watawajua wapinzani wao.
  Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Tottenham walishinda dhidi ya PSG kwa matuta baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
  Thrilling tie: Chelsea held out with 10 men and then doubled their lead at the end
  Mtifuano: Chelsea waliizima Barca wakiwa 10 uwanjani.
  Thrilling tie: Chelsea held out with 10 men and then doubled their lead at the end
  Alikuwa ni mchezaji wa Spurs, Shaquille Coulthirst aliyeanza kufunga bao kwenye pambano hilo lakini PSG walichomoa bao hilo kupitia kwa Alexis Sainrimat, kabla ya matokeo kuamuliwa kwa penalty na Spurs wakashindwa kwa penalti 4-3.
  Kwa upande Liverpool walitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Sporting CP pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Estadio Alvalade.
  Carlos Mane alifunga mara mbili huku Joao Palhina na Wilson Manafa wakiongeza mabao mengine.

  Through: Tottenham defeated PSG on penalties to make it to the quarter-finals
  Kitu: Tottenham walishinda kwa penalti dhidi ya PSG

  Through: Tottenham defeated PSG on penalties to make it to the quarter-finals
  Through: Tottenham defeated PSG on penalties to make it to the quarter-finals

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHELSEA YAIFUMUA BARCELONA 2-0 KOMBE LA VIJANA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top