• HABARI MPYA

    Tuesday, February 26, 2013

    MESSI NA RONALDO NI CHUI NA PAKA


    NI Wachezaji Bora Duniani lakini hawawezi kuja kuwa marafiki wa karibu. Wakati Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanakutana leo usiku, watasalimiana kidogo tu lakini hakuna kitu cha ziada kati yao.
    Wanatakiwa kupongezana. Kila wakati Ronaldo akifanya vizuri akiwa na Real Madrid, Messi hujaribu kufanya vizuri zaid kwa Barcelona. Matokeo ya upinzani wao yamekuwa makubwa sana na yanamaanisha kwamba soka la Hispania kwa sasa ni zuri kutazama.
    Lakini watazame leo kwenye mechi ya pili ya nisu fainali ya Kombe la Mafalme – na kwa mara nyingine tena Jumamosi kwenye La Liga, hutaona kitu cha ziada zaidi ya kupenana mikono tu. Hutakiwi kuwa mtaalamu wa kusoma lugha ya viungo kujiua kwamba wawili hawa hawapendani.

    Head to head: This era's greatest two football players, Cristiano Ronaldo (left) and Lionel Messi (right)

    Uso kwa uso: wakati wa wachezaji bora wawili, Cristiano Ronaldo (kushoto) na Lionel Messi (Kulia)
    Competition: Would Messi be quite as good without Ronaldo to spur him on?

    Mashindano: Je, Messi angekuwa bora hivi bila upinzani wa Ronaldo?

    Ni swali ambalo kila mtu anatakiwa kujiuliza, ni hili: ningekuwa wapi mimi bila wewe?
    Unatakiwa kuhoji kama takwimu zao zingekuwa za kuvutia, iwapo wangekuwa wanacheza ligi tofauti. Ronaldo alipofunga hat-trick mwezi uliopita dhidi ya Getafe, Messi alifunga mabao manne usiku uliofuata dhidi ya Osasuna. 
    Kilichokosekana siku hiyo ni kwa Messi kufunua fulana yake na kusema ‘kila unacheweza kufanya mimi ninakiifanya vizuri zaidi yako’.
    Messi siku zote amekuwa mchezaji wa kiwango cha juu duniani na amezungukwa na wachawi wawili Xavi na Andres Iniesta lakini unaweza kusema kwamba uhamisho wa pauni milioni 80 wa Ronaldo kutoka Manchester United mwaka 2009, kwa kiasi fulani ulipandisha takwimu zake.
    Strength to strength: Since leaving Manchester United, Ronaldo has pushed on further

    Kiwango: toka aondoke Manchester United, Ronaldo amekuwa akiongeza kiwango chake siku hadi siku

    Kama ukiangalia jinsi Messi alivyotimiza mabao 300, mabao yake ya kwanza 80 aliyapata katika mechi 161, wakati amefunga mabao 221, katika mechi 204 tangu Ronaldo atue Bernabeu, kiwango ambacho kimemfanya awe mmoja kati ya wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa.
    Ronaldo, kwa upande wake hawezi kukuri hili, lakini katika harakati zake za kumpita Messi ametokea kuwa bora sana duniani, akiwa Man United alifunga mabao 118 katika mechi 292, lakini akiwa Real Madrid amefunga mabao 183 katika mechi 182.
    Ugomvi wake na Messi ulionekana wakati wa majira ya joto mwaka jana kwenye michuano ya Euro 2012, pale Mashabiki wa Denmark walipokuwa wakimponda kila anapogusa mpira na kutaja jina la Messi.
    “Unajua wapi alikuwa muda kama huu mwaka jana,” alihoji Ronaldo baada ya mechi. “alikuwa akitolewa kwenye michuano ya Copa America. Akiwa na timu yake ya taifa. Hilo ni baya siyo?”
    Ushahidi mwingine ulikuja wakati wa upigaji kura wa tuzo ya Ballon D’Or, ambayo Messi alishinda kwa mara ya nne mfululizo. Kama nahodha wa Argentina Messi aliwapigia kura Iniesta, Xavi na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Falcao. 
    Ronaldo, kwa upande wake alipata nafasi ya kupiga kura, akiwa kama nahodha wa Ureno, alikataa jukumu hilo na kumpa msaidizi wake Bruno Alves. Haikuwa ajabu, Alves alimpigia Ronaldo kama namba moja wake na kumtosa Messi kwenye orosha yake.
    Sawa uadui kwenye michezo siyo jambo jipya. Waangalie  Sebastian Coe na Steve Ovett. Je, Coe angeshinda medali ya dhahabu ya mita 1500 jijini Moscow mwaka 1980, kama isingekuwa kuzidiwa na Ovett siku sita kabla kwenye mita 800?
    Ushindani kati ya wawili hao ndio ulikuwa sababu ya kuwa na kizazi cha dhahabu Uingereza kwenye riadha katika miaka ya 1980, Coe aliwahi kusema kwamba upinzani wake na Ovett ulikuwa ni moja kati ya sababu za yeye kuvunja rekodi ya dunia mara tatu katika siku  41, mwaka 1980.
    Pia hakukuwa na mapenzi kati ya Ayrton Senna na Alain Prost ambao walitawala mbio za mgari za Formula One.
    Fierce rivalry: Alain Prost (left) and Ayrton Senna (centre) were driven by each other

    Upinzani mkubwa: Alain Prost (kushoto) na Ayrton Senna (kati kati) walikuwa wapinzani wakubwa


    Je, Wangeweza kushinda mashindano mengi kama isingekuwa ushindani mkali kati yao? Senna, alijulikana kama mtu asiyemuoga kwa sababu Prost alikuwa akimlazimisha kufanya hivyo.
    Janga lilitokea katika upinzani wao baada ya Senna kufa mwaka 1994 na Prost alisema sehemu yake pia ilikuwa siku hiyo, pamoja na Senna.
    Hawakuwa marafiki barabarani, lakini heshima aliyokuwa nayo Prost kwa Senna ilionekana pale alipohudhuria kikamilifu mazishi yake.
    Pia ni kuhusu kukubaliana na kutambuana. Victoria Pendleton na Anna Mears, wanawake waliotawala mbio za baiskeli, walikuwa maadui wakubwa lakini uadui wao ulikwama sekunde ya mwisho ya mashindano ambayo Mears alishinda walikumbatiana mwisho wa shindano hilo, ilikuwa wakati wa mashindano ya Olimpiki mwaka jana.
    Seb Coe shakes Steve Ovett's hand
    Anna Mears leads Great Britain's Victoria Pendleton
    Seb Coe akimpa mkono, Steve Ovett (Kushoto) Victoria Pendleton akiwanyuma ya Anna Mears


    Hawa walikuwa wanamichezo wawili ambao walitambua sehemu ya kila moja kwenye mafanikio ya mwenzake na wakaamua kuachana na uadui wao.
    Nini kitatokea kwa Ronaldo na Messi? Hawawezi kupatana. Ronaldo alipigwa picha akiwa kanuna pale Messi aliposhinda tuzo ya Ballon D’Or. Messi, kwa upande wake hajawahi kusema wazi wazi ni kiasi gani Ronaldo ni mchezaji mzuri. Uadui wao ni mkubwa kuliko kuheshimiana kwao.
    Je, hilo linatakiwa kubaki hivyo, itakuwa aibu sana. Wote wawili wanacheza na wachezaji wazuri sana na wamekuwa wakilindwa na makocha bora, lakini wanatakiwa pia kuheshimu upinzani wao, kwa sababu uwawafanya wacheze vizuri zaidi, na labda vizuri zaidi hata walivyowahi kuota.
    Kwa hiyo, wakati ambao hawawezi kuishi pamoja – lakini ni wazi hawawezi kuishi mbali mbali.
    No eye contact: Ronaldo and Messi barely look at each other as they shake hands

    Hawaangaliani usoni: Ronaldo na Messi wanapeana mikono huku hawaangaliani usoni
    Three's company: Ronaldo (left) and Messi (right), separated by Andres Iniesta

    Mapacha watatu: Ronaldo (kushoto) na Messi (Kulia), kati kati yao yuko Andres Iniesta
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MESSI NA RONALDO NI CHUI NA PAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top