• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 22, 2013

  HUYU NI MHUJUMU TIMU, AU?

  Beki wa timu ya soka ya Azam FC, Erasto Nyoni anayetumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana na klabu yake, kwa tuhuma za kuhusika kuihujumu timu hiyo katika mechi dhidi ya Simba SC, mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Picha hii ilipigwa jana wakati wa sherehe za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars kukabidhi basi la timu hiyo, makao makuu ya kiwanda cha kampuni hiyo, Ilala, Dar es Salaam.
  Nyoni ambaye amekumbwa na adhabu hiyo kwa pamoja na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki wenzake, Aggrey Morris na Said Mourad, aliwawakilisha wachezaji wenzake wa Taifa Stars jana, ambao kwa kipindi hiki wamebanwa na majukumu ya klabu zao.
  Tazama mara mbili sura yake, je unaweza kukubali huyu jamaa alicheza mchezo huo mchafu, au jumba bovu tu lilimdondokea? 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: HUYU NI MHUJUMU TIMU, AU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top