• HABARI MPYA

    Tuesday, February 19, 2013

    HAYA SASA KITU CHA NZAGAMBA HICHOOOO

    Kushoto ni Mkurugenzi wa kinywaji cha Nzagabwa Kiroi Suma akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo Kulia alipo tembelea kiwanda hicho katikati ni Mkuu wa kiwanda cha Nzagamba Bw. Patrick Phiri.

    Na Mwandishi Wetu
    KIWANDA kipya cha kuzalisha bia ya asili ijulikanayo Nzagamba kimefunguliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evaristi Ndikilo.
    Kiwanda hicho ambacho kipo chini ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kitajihusisha na kutengeneza bia hiyo ya asili, ambayo tayari imeanza kupokelewa kwa shangwe na wenyeji wa Kanda ya Ziwa.
    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho, Mhandisi Ndikilo alisema, amefarijika mno kuona kimejengwa Mwanza, kwani kitachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya mkoa huo.
    “Niwapongeze sana wenzetu wa Nzagamba kwa kuja na wazo zuri kama hili la kuanzisha bia ya asili, tena wakaipa jina lenye asili ya Kanda ya Ziwa hususani kabila la Wasukuma.
    “Hii imenifurahisha. Lakini kikubwa zaidi ni uamuzi wa kukiweka kiwanda hiki hapa Mwanza, kwa sababu mlikuwa na uwezo wakuamua kujenga mkoa mwingine wowote ule lakini mkatoa upendeleo wa dhati kwa mkoa wetu. Kwa uamuzi huo tunashukuru sana,” alisema.
    Aliwataka wananchi kuhakikisha wanaonyesha uzalendo wa dhati kwa kupenda kutumia vitu vya asili, huku akitolea mifano ya nchi za Zambia na Malawi, ambapo bia za asili zinapewa nafasi kubwa.
    Mkurugenzi wa Kiwanda cha Nzagamba, Kirowi Suma naye alisema watahakikisha wanazalisha bidhaa bora zaidi na kuwataka Watanzania wapende vitu vya asili ili kuonyesha uzalendo wao.
    “Kwetu Nzagamba tunaamini tutaendelea kupigania ubora wa bidhaa yetu na naomba Watanzania watuunge mkono kwa kuipa nafasi bia hii ya asili,” alisema Suma.
    Nzagamba tayari imeanza kusambazwa, huku ikipokelewa vizuri zaidi na watumiaji, kutokana na kuwekwa katika ubora unaotakiwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HAYA SASA KITU CHA NZAGAMBA HICHOOOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top