• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 28, 2013

  RONALDO ATAUNGANA TENA NA FERGUSON?


  SIR Alex Ferguson amemuita ‘hanunuliki’ na kocha huyo wa Manchester United atakuwa aliona kiwango cha Cristiano Ronaldo alipokuwa akiua Barcelona, Nou Camp, Jumanne usiku kwa kufurahishwa nae na kumuogopa.
  Ferguson anajua wazi kwamba anatakiwa kutafuta njia mbadala ya kumzuia mshambuliaji huyo wa Real Madrid atakapokuja Old Trafford wiki ijayo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Lakini, wakati Man United wakijipanga kumkabili Ronaldo, tangu alipoondoka kwa ada ya pauni milioni 80 na kujiunga na Real Madrid miaka mine iliyopita, kumekuwa na mjadala wa Mreno huyo kurudi Old Trafford.

  Manchester calling? Cristiano Ronaldo has starred for Real Madrid but could yet return to the Premier League
  Manchester wanamuita? Cristiano Ronaldo amefanya vizuri akiwa na Real Madrid lakini bado anaweza kurudi Ligi Kuu ya England

  Wengi wanaweza kuhisi haiwezekani. Ferguson anasema haamini kama hilo litatokea, japokuwa aliwahi kusema maneno kama hayo kwa Robin van Persie. 
  Lakini kuna maono ndani ya klabu kwamba dili la Ronaldo siyo la kusadikika kama wengi wanavyodhani.
  Kwa mujibu wa Sportsmail, klabu hiyo imeshalichunguza suala la kununua mchezaji wa bei mbaya sana kwenye historia ya klabu hiyo – Ferguson anahisi watalazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 100.
  Baada ya kumuuangalia Ronaldo akifunga mara mbili dhidi ya Barca, Jumanne na kufikisha idadi ya mabao 185 katika mechi 183, kocha huyo wa Man United anajua kwamba Ronaldo ni mmoja kati ya wachezaji ambao wanahadhi ya kununuliwa kwa fedha hiyo.
  Ferguson aliacha miliango wazi pale alipoulizwa kuhusu Ronaldo, Disemba, alisema: “Huwezi kujua. Atataka kuhama siku moja natumaini atataka kuja hapa.

  Then and now: Sir Alex Ferguson has never hidden his admiration for Ronaldo after guiding his career
  Zamani na sasa: Sir Alex Ferguson hajawahi kuficha mapenzi yake kwa Ronaldo 

  Then and now: Sir Alex Ferguson has never hidden his admiration for Ronaldo after guiding his career
  “Ningependa kuona hilo lakini ni mawazo ya kusadikika. Kwanza kuna hili la kiasi gani kitatumika kumtoa Real Madrid na la pili sidhani kama kuna uwezekano wa kuuza.”
  Kama – Ronaldo ataamua kuondoka Bernabeu kabla ya kumalizika kwa mkataba wake mwaka 2015, Man United wanaamini litakuja suala la kuchagua kati ya Paris Saint-Germain na Man United na wanaamini atachagua Old Trafford.
  Manchester City hawatakiwi kusahaulika, lakini Man United watakuwa chaguo la kwanza kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa mwaka 2009 wakati akitua Real Madrid na rekodi yake ya uhamisho bado haijavunjwa. Man United wanaweza kulipa kiasi cha pauni milioni 60 kumnunua Ronaldo, japokuwa kiwango chake kimekuwa, lakini kwa sasa anamiaka 28 na amebakiza miaka miwili tu kwenye mkataba wake na Real Madrid.
  Mshahara wake unaweza kufikia hadi kiasi cha pauni milioni 100, lakini wanajua jinsi gani mchezaji huyo anafaida kwao kibiashara.

  On the money: Ronaldo scored twice as Real Madrid knocked Barcelona out of the Copa del Rey on Tuesday
  Pesa: Ronaldo alifunga mara mbili wakati Real Madrid walipowatoa Barcelona kwenye michuano ya Kombe la Mfalme

  Kiongozi ajae wa Old Trafford, Ed Woodward anatajwa kuwa kipenzi cha kusajili wachezaji wenye majina makubwa ilikuvutia kibiashara duniani, pia Man United wanaweza kuangalia jinsi jina lao linavyokuwa duniani.
  Miamba hiyo ya Ligi Kuu ya England pia inajua wazi kwamba wanawachezaji ambao wanaivutia Madrid na watawatumia kuongeza nguvu kwenye usajili. David de Gea, anathaminiwa sana Hispania wakati Nani na Javier  Hernandez wanaweza kutumika kama chambo.
  Mipango ya Man United bado iko mkwenye hatua za awali sana na Real Madrid wanajua kuwa Ronaldo anatakiwa Old Trafford. Lakini dili yoyote itafanyika ikiwa tu, Ronaldo atakuwa tayari kupunguza mapenzi yake na Real Madrid jambo ambalo bado halijawa wazi.
  Aliongelea kuhusu kujiona hapendeki Hispania na Real Madrid, kutokana na klabu hiyo kugoma kuanza kuzungumza nae juu ya mkataba mpya wakati Lionel Messi amesaini mkataba mnono Barca.

  Poised: Ronaldo scored against United at the Bernabeu ahead of the second leg in Manchester next week
  Kaganda: Ronaldo akifunga dhidi ya Man United, Bernabeu

  Poised: Ronaldo scored against United at the Bernabeu ahead of the second leg in Manchester next week
  Ronaldo amesema kwamba atahakikisha anamaliza mkataba wake, lakini haiwezekani Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akaruhusu hilo kutokea. Majadiliano ya mkataba mpya yanatarajiwa kuanza mwisho wa msimu huu huku Perez akiwa kwenye presha ya uchaguzi utakao kuwa Juni mwaka huu.
  Hatahivyo, kutokana na kukosa mshindani Perez anaweza kupata muda mwingi zaidi wa kuchakachua, Jana, Real Madrid walianza majadiliano na Napoli, Juu ya Edinson Cavani, na kama Perez atafanikiwa kumchukua Gareth Bale, Ronaldo anaweza kufunguliwa milango.
  Ferguson alisema: “Nadhani Real Madrid  wanajaribu kwa hali na mali kumsainisha mkataba mpya na nadhani hilo linatokea.”
  Wanaweza kuwa wamepatia, Man United watakuwa na mpango wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RONALDO ATAUNGANA TENA NA FERGUSON? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top