![]() |
| Mtakatifu Ton na Bin Zubeiry |
Na Mahmoud Zubeiry
KIZURI
chajiuza. Naam, habari ndiyo hiyo. Kocha Mbelgiji Tom Saintfiet aliyefukuzwa
Yanga baada ya siku 80 za kuwa kazini, amepata mkataba wa kuifundisha timu ya
taifa ya Yemen kuanzia mwezi huu.
Akizungumza na
BIN
ZUBEIRY kutoka Sana’a, Yemen mida hii, Mtakatifu Tom alisema kwamba
anatarajia kuiongoza timu hiyo ya Magharibi mwa bara Asia katika michuano ya Kombe
la Mataifa ya Magharibi mwa Asia (kama Kombe la Challenge la CECAFA)
itakayofanyika nchini Kuwait Desemba mwaka huu.
Alisema katika
michuano hiyo, amepangwa kundi moja na Saudi Arabia, Iran na Bahrain na Januari
mwakani, ataiongoza timu hiyo katika Kombe la Gulf huko Bahrain.
“Kwa sasa
nipo katika Jiji la Sana'a na kesho nitaanza kazi kwa kambi ya kujiandaa na
mchezo wa kirafiki Beirut, Oktoba 16 dhidi ya Lebanon,”alisema Mtakatifu Tom.
Saintfiet
alifukuzwa Yanga baada ya kutofautiana misimamo na uongozi wa Yanga, akiwa
amefanya kazi siku 80 na kuiachia timu taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame.
Saintfiet amefungwa
mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo,
Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu (Kirafiki) 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi, Kagame) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan, Kagame) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame) 1-1 (5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam (Kagame) 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon (Kirafiki) 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda) 2-0
10.
Yanga
Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda) 2-1
11.
Yanga
Vs Coastal Union (Kirafiki) 2-1
12.
Yanga
Vs Moro United (Kirafiki) 4-0
13.
Yanga
Vs Prisons (Ligi Kuu) 0-0
14.
Yanga
Vs Mtibwa (Ligi Kuu) 0-3



.png)
0 comments:
Post a Comment