• HABARI MPYA

    Wednesday, February 15, 2012

    DAKTARI WA WHITNEY MATATANI

    NEW YORK, Marekani
    DAKTARI wa Whitney Houston anatakiwa kutoa maelezo sahihi kama anajua kuwa mwanamuziki huyo alikuwa akitumia vidoge vya kupunguza maumivu vilivyosababis kifo chake.
    Nyota huyo alikufa kabla ya kuzama kwenye sinki la bafuni kwenye hoteli ulipokutwa mwili wake. Inadhaniwa mwanamuziki huyo amekufa baada ya kuchanganya kwa pamoja dawa na pombe kuliko kule kunywa maji kwenye sinki ulipokutwa mwili wake.
    Nyota huyo wa filamu ya The Bodyguard alikutwa amekufa kwenye bafu la hoteli ya Beverly Hilton huku uso wake ukiwa ndani ya sinki la kuogea Jumamosi iliyopita.
    Bado kuna kizunguzungu juu ya sababu ya kifo cha nyota huyo. Kwa mujibu wa taarifa ya familia ya mwanamuziki huyo ilisema Whitney alikufa kabla ya kuzama kwenye maji baada ya kunywa dawa mbalimbali na pombe.
    Chupa ya dawa iliyopatikana juzi usiku kwenye chumba chake ni sawa na ile aliyokunywa Michael Jackson.
    Askari walisema dawa hizo ni kutoka katika kampuni ya Mickey Fine chemists. Ndiko aliponunua Jacko. Pia kuna habari kwamba Whitney alipatwa na ugonjwa wa moyo kutokana na madhara ya mchanganyiko wa dawa hizo.
    Inaaminia kiasi kidogo cha maji kilikutwa kwenye mapafu yake. Askari wa Los Angeles walipofanya uchunguzi wao walisema walikuta chupa sita za dawa aina ya Xanax, Lorazepam, Ibuprofen, Midol, Amoxicillin na Valium.
    Pia, picha zilizotolewa jana zilionyesha chakula alichokula Whitney muda mfupi kabla kifo chake. Nyota huyo alikuwa ameagiza hamburger, fries, turkey sandwich na jalapenos, kwa mujibu wa ripoti.
    Alikuwa amekula burger na chipsi, lakini aliamua kwenda kupumzika bafuni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAKTARI WA WHITNEY MATATANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top