• HABARI MPYA

    Friday, May 12, 2017

    SINGIDA UNITED KUSAJILI WENGINE WATATU WA KIGENI

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
    SINGIDA United imesema itasajili wachezaji wengine watatu wa kigeni ili kukamilisha idadi ya wachezaji saba kwa mujibu wa kanuni za usajili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Mratibu wa Singida United, Sanga Festo alisema kwamba baada ya kukamilisha usajili wa beki Mganda Shafik Batambuze mwenye umri wa miaka 23 aliyesaini mkataba wa miaka miwili kutoka Tusker FC ya Kenya, sasa wanaelekeza nguvu zao katika kusaka wengine watatu.
    Beki Mganda Shafik Batambuze (kulia) mwenye umri wa miaka 23 ametua Singida United kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Tusker FC ya Kenya 

    Ikumbukwe tayari Singida United imekwishasajili wachezaji watatu kutoka Zimbabwe, ambao ni Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu.
    Sanga amesema kwamba wamemsajili Batambuze baada ya kuridhishwa na uwezo wake kufuatia kuwamo katika kikosi cha Uganda kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu nchini Gabon.
    Sanga alikwenda Nairobi Jumatatu hii kwa ajili ya kumalizana na mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa ni mchezaji bora wa ligi ya Kenya na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa Tusker wa FA CUP na Ligi Kuu.
    Timu hiyo ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja msimu huu kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao nyinge ni Njombe Mji na Lipuli FC ya Iringa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA UNITED KUSAJILI WENGINE WATATU WA KIGENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top