• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2017

  MAREFA WA MAGHARIBI WATUPU KUCHEZESHA SERENGETI BOYS NA NIGER KESHO

  Na Mahmoud Zubeiry, PORT GENTIL
  MAREFA wa Afrika Magharibi watupu wamepangwa kuchezesha mechi ya mwisho ya Kundi B Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa 17 kati ya Tanzania na Niger kesho Uwanja wa Port Gentil, Gabon.
  Marefa hao ni Daniel Nii Ayi Laryea wa Ghana atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Seydou Tiama wa Burkina Faso na Mamady Tere wa Guinea katika mchezo utakaoanza Saa 12:30 kesho.
  Tanzania inahitaji sare tu kujihakikishia kwenda Nusu Fainali na pia kufuzu Kombe la Dunia baada ya sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Mali na ushindi wa 2-1 dhidi ya Angola ambazo nazo zitamenyana kesho muda huo huo Uwanja wa l’Amittiee mjini Libreville.
  Mechi za Kundi A zitaanza kuhitimishwa leo na Cameroon itajaribu kuungana na Ghana kufuzu Nusu Fainali, itakapomenyana na vibonde wenzao, wenyeji Gabon kuanzia Saa 12:30 jioni Uwanja wa Port Gentil.
  Cameroon watahitaji kuifunga Gabon leo baada ya kufungwa 4-0 na Ghana na kutoa sare ya 1-1 na Guinea katika mechi zake zilizotangulia, huku wakiiombea dua mbaya Guinea ifungwe na Black Starlets ili wao waende Nusu Fainali. Ghana na Guinea zitamenyana kuanzia Saa 12:30 pia Uwanja wa l’Amittie mjini Libreville. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAREFA WA MAGHARIBI WATUPU KUCHEZESHA SERENGETI BOYS NA NIGER KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top