• HABARI MPYA

    Friday, May 19, 2017

    ANDER HERRERA AWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MAN UNITED

    Kipa David de Gea akimkabidhi Ander Herrera tuzo ya Sir Matt Busby ya Mchezaji Bora wa Mwaka PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    WASHINDI WA TUZO 

    Mchezaji Bora wa Mwaka tuzo ya Sir Matt Busby 
    Ander Herrera 
    Mchezaji Bora wa Wachezaji 
    Antonio Valencia
    Bao Bora la Msimu 
    Henrikh Mkhitaryan
    Mchezaji Bora Chipukizi 
    Angel Gomes 
    Mchezaji Bora wa Timu ya Wachezaji wa akiba
    Axel Tuanzebe 
    KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amempiku mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na winga Antonio Valencia na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu katika sherehe za tuzo zilizofanyika Uwanja wa Old Trafford Alhamisi usiku.
    Kwa kura zilizopigwa na mashabiki hakukuwa na mshindi kabisa, kwani wachezaji wawili wa juu walitenganishwa na kura 20 hadi saa za mwisho za upigaji kura kwa mujibu wa tovuti ya Manchester United
    Lakini Herrera akafanikiwa kuibuka mshindi baada ya kazi nzuri aliyoifanya katika kiungo msimu huu, huku Valencia akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Mwaka kama kupata suluhu, huku Ibrahimovic akiondoka mikono mitupu licha ya kuwa na msimu mzuri pia.
    Herrera alisema: "Ni maalum sana kwangu kushinda tuzo hii, kwa sababu ukiona orodha ya washindi unaona ni muhimu kiasi gani...na kwa sababu nimezuia rekodi ya David [de Gea] na kwa vizuri zaidi kwa sababu tuzo inabaki Hispania,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANDER HERRERA AWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top