• HABARI MPYA

    Wednesday, May 17, 2017

    45 WAITWA KUWANIA NAFASI TWIGA STARS

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Sebastian Nkoma ameita wachezaji 45 kwa ajili ya mchujo wa kupata nafasi ya kujiunga na kikosi cha timu hiyo kitakachosriki mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Ghana mwaka 2018.
    Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba wachezaji hao wataingia kambini Mei 21 hadi 27 kwa ajili ya kuangaliwa na watakaoonyesha uwezo watachukuliwa kikosi cha Twiga Stars.
    Madadi, kocha wa zamani wa klabu ya Simba, amesema kwamba baada ya kupatikana wachezaji wa kuongezwa Twiga Stars, kambi rasmi ya maandalizi ya mechi za kufuzu AFCON ya Ghana mwakani itaanza Septemba au Oktoba, mwaka huu.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikuwepo kwenye fainali ya Ligi ya Taifa ya Wanawake
    Amesema lengo si kukata titeti ya kushiriki fainali za AFCON za Ghana tu, bali pia na kupata nafasi ya kwenda Kombe la Wanawake Ufaransa mwaka 2019.
    Wachezaji walioteuliwa na kocha Sebastian Nkoma kwa ajili ya kuwania nafasi ya kuingia kikosi cha Twiga Stars kufuatia kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya Taifa miezi miwili iliyopita ni; Agatha Joel, Ever Jackson, Christina Daudi, Shamim Khamis, Saada Ramadhani, Oprah Clement, Faraja Kimula, Zubeda Juma, Irene Mkundila, Veronica Mazanda, Christina Pangrasi, Aisha Hamza, Emil Mdim, Semeni Hussein na Mgeni Kisuda.
    Wengine ni Daclina Mwisigao, Esther Mayala, Enekia Yona, Herieth Shijja, Janeth Petro, Arafa Omar, Elizabeth Nashon, Zainab Abdallah, Rehema Butene, Zainab Mlenda, Hadija Mohammed, Grace Mbelay, Aquila Gasper, Shan Sultan na Rukia Anafi.
    Wengine ni Zuena Aziz, Amina Ramadhani, Neema Paul, Rehema Abdul, Kapangara Kingamkono, Asha Malaigwa, Antoneka Mbunga, Sylvia Mwacha, Aisha Mbabaje, Rukia Magi, Hawa Suleiman, Amina Abdallah, Saida Muhaji, Mwamvita Muba na Oliver Lyimo.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 45 WAITWA KUWANIA NAFASI TWIGA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top