• HABARI MPYA

  Monday, November 07, 2016

  RONALDO AONGEZA MIAKA MITANO REAL NA KUSEMA; "NITACHEZA HADI MIAKA 41"

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na Real Madrid leo Jumatatu na kusema kwamba amebakiza miaka 10 ya kuendelea kucheza soka ya ushindani.
  Kijana huyo wa umri wa miaka 31 amesaini hadi mwaka 2021, lakini akasema katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu kwamba anataka kustaafu akiwa ana umri wa miaka 41.
  Ronaldo ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo, akipata mshahara wa Pauni 365,000 kwa wiki ambao haujabadilika katika mkataba mpya. 
  Tayari ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu na kama atamaliza mkataba wake, basi atakuwa amedumu kwenye klabu hiyo kwa misimu 12 Bernabeu – msimu mmoja zaidi ya gwiji wa muda wote wa klabi, Alfredo Di Stefano.

  Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema anataka kucheza hadi akiwa ana umri wa miaka 41 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MATAJI ALIYOSHINDA RONALDO REAL MADRID 

  La Liga: 2011–12
  Copa del Rey: 2010–11, 2013–14
  Super Cup ya Hispania: 2012
  Ligi ya Mabingwa: 2013–14, 2015–16
  Super Cup ya UEFA: 2014
  Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2014
  Alisema: "Hii ni siku maalum kwangui, kuongeza muda wangu wa kuwa na klabu, klabu iliyo katika moyo wangu. Kusaini mkataba mpya wa miaka mitano ni maalum sana na acha iwe wazi, huu si mkataba wa mwisho,".
  "Nataka kuendelea kuweka historia na nina uhakika kwamba miaka mitano mingine nitaendelea kufunga mabao na kushinda mataji na klabu bora duniani. Nataka kumalizia soka yangu katika klabu hii,"
  Alipoulizwa kama anataka kuvunja rekodi ya Ferenc Puskas aliyecheza hadi ana miaka 39, Ronaldo anayetaka kufunga mabao 500 Real Madrid, alisema: 'Arobaini na moja,' na alipoulizwa amebakiza muda gani akasema: "Nafikiri nimebakiza miaka 10,".

  WACHEZAJI 10 WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI 

  1= Cristiano Ronaldo (Real Madrid) Pauni 365,000 kwa wkiki Pauni Milioni 19 kwa mwaka
  1= Lionel Messi (Barcelona) Pauni 365,000 kwa wiki Pauni Milioni 19 kwa mwaka
  3 Gareth Bale (Real Madrid) Pauni 346,000 kwa wiki, Pauni Milioni 18 kwa mwaka
  4 Hulk (Shanghai SIPG) Pauni 317,000 kwa wiki Pauni Milioni 16.5 kwa mwaka
  5 Paul Pogba (Manchester United) Pauni 290,000 kwa wiki Pauni Milioni 15 kwa mwaka
  6 Neymar (Barcelona) Pauni 289,000 kwa wiki Pauni Milioni 15 kwa mwaka
  7= Graziano Pelle (Shandong Luneng) Pauni 260,000 kwa wiki Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka
  7= Wayne Rooney (Manchester United) Pauni 260,000 kwa wiki, Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka
  9 Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) Pauni 250,000 kwa wiki, Pauni Milioni 13 kwa mwaka
  10= Sergio Aguero (Manchester City) Pauni 240,000 kwa wiki, Pauni Milioni 12.5 kwa mwaka
  10= Yaya Toure (Manchester City) Pauni 240,000 kwa wiki, Pauni Milioni 12.5 kwa mwaka
  Makadirio yote haya ni kabla ya makatbo ya kodi na wengine wanaweza kuwa wananufaika zaidi na posho mbalimbali 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AONGEZA MIAKA MITANO REAL NA KUSEMA; "NITACHEZA HADI MIAKA 41" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top