BONDIA Muingereza anayechipukia vizuri katika uzito wa juu, Anthony Joshua ameendeleza wimbi lake la ushindi wa Knockout, baada ya usiku wa jana kushinda KO ya 12 mfululizo dhidi ya Zumbano Love.
Joshua, anayefananishwa ne bingwa wa zamani wa dunia uzito wa juu, Muingereza mwenzake, Lennox Lewis alimmaliza Zumbano katika raundi ya pili tu mjini Birmingham jana.
Baada ya ushindi huo, Joshua aliyeacha ngumi za Ridhaa baada ya kushinda Medali ya Dhahabu ya Olimpiki, atarejea ulingoni Mei 30 kuzipiga na mkongwe Kevin Johnson.
Bondia Zumbano Love akiwa amesinzia 'sakafuni' baada ya kuangshwa na ngumi ya Anthony Joshua 'New Lewis' jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment